Monday, February 24, 2014


WABUNGE WALILIA NYONGEZA YA POSHO


Hali ya ubinafsi na msemo wa Kiswahili wa aliyeshiba hamjui mwenye njaa ilijitokeza siku chache baada ya Bunge Maalum la Katiba kuanza mjini Dodoma.

Imekuwa kawaida kwa wananchi wanaposikia kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiomba kuongezewa posho hulalama kuwa wanajineemesha wao na kuwaacha wapigakura wao wakisota kwa ugumu wa maisha.

Wakijadili rasimu ya kanuni za bunge, wajumbe kadhaa walitaka waongezewe posho kwa kile walichodai ni kupanda kwa gharama za maisha tangu kuanza kwa mkutano huo.

Wajumbe hao waliomba kiwango wanachppewa sasa cha Sh 300,000 kwa siku kiongezwe kwa kuwa hakiwatoshi, hivyo wakapendekeza kiongezwe ili kiweze kukidhi mahitaji muhimu.

0 Responses to “ ”

Post a Comment

More to Read