Thursday, March 13, 2014

MTIKILA : HIVI MWENYEKITI HUNA HOFU YA MUNGU.


Mchungaji Christopher Mtikila


Mchungaji Christopher Mtikila ametuhumu mwenyekiti wa muda wa bunge maalum la katiba , pandu ameir kificho kwamba hana hofu ya Mungu kwa kumnyima haki yake ya kuzungumza bungeni.

Hayo yalitolewa juzi asubuhi wakati wajumbe wa bunge maalum wakipitisha azimio la kuridhia  rasimu ya mwisho ya kanuni za bunge hilo. Kanuni hizo zilipitishwa kwa kauli moja juzi baada ya mwenyekiti wa kamati  ya kushauri na  kutoa mapendekezo  juu ya maboresho ya rasimu ya kanuni profesa costa  mahalu kuwasilisha hoja ya kupitisha azimio hilo bungeni.

Wajumbe 13 kutoka karibu kila kundi lililohusika kuunda bunge hilo, walizungumza kwa idhini ya kificho , ndipo baada ya mchangiaji wa mwisho  askofu amos mwagache   kumaliza na kificho kuanza kuhitimisha mjadala huo, ikaibuka sauti kutoka ndani ya ukumbi huo.

“Mwenyekiti kwanini unizuia kuzungumza? Niliyonayo hayawezi kunufaisha nchi? Nataka uniambie kwanini unaninyima haki yangu? Haki inatajwa sana hapa ndani  hata amri ya Mungu inahimiza kutenda haki hun ahofu ya Mungu ndiyo maana unaninyima haki yangu” alisema mchungaji Mtikila na kuongeza:

“Mwenyekiti unataka wajumbe wazungumze unayotaka kusikia hii ni kumkosea Mungu kusema ni haki yangu na  mimi nina neno la kusema niache nizungumze.  


0 Responses to “MTIKILA : HIVI MWENYEKITI HUNA HOFU YA MUNGU.”

Post a Comment

More to Read