Thursday, March 13, 2014

WABAYA WAMENIZUSHIA UGONJWA, ASEMA SITTA.


Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta



Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta amesema taarifa zilizosambaa juzi usiku kuwa yu mahututi na kwamba amepelekwa hospitalini zilitolewa na wabaya wake wanochukia msimamo wake.

Amesema yeye ni kiongozi anayetenda haki kwa watu wote na kwamba jambo hilo lina wachukiza baadhi ya watu  wote na kwamba jambio hilo linawachukiza baadhi ya watu ambao wanataka kupendelewa katika kila jambo.

Juzi uliibuka uvumi kuwa sitta aliyechaguliwa kwa kishindo jana kuwa mwenyekiti wa bunge maalum la katiba aliugua ghafla kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwenyekiti wa bunge hilo.

Akizungumza katika mahojiano maalum nyumbani kwake mjini Dodoma jana sitta amesema “wabaya wangu ndiyo waliosambaza taarifa hizo . mimi ni mzima na leo (jana) saa 2:32 asubuhi nilirusha fomu za kugombea nafasi ya uenyekiti.

Sitta amesema hakushangazwa na taarifa hizo kwa sababu alipoteuliwa na CCM kugombea nafasi hiyo wapo waliopinga na kusema hawezi kugombea kwa sababu yeye ni waziri.

“Watu wengine wakadai mimi na Andrew change aliyetaka kugombea kuwa tulikuwa tunakigawa chama  niliwajibu wakati wa uchaguzi lazima watu wagawanyike “ alisema sitta.

Katika uchaguzi wa jana sitta  alimshinda mgombea mwenzake , Hashimu Rungwe.

0 Responses to “WABAYA WAMENIZUSHIA UGONJWA, ASEMA SITTA.”

Post a Comment

More to Read