Monday, March 17, 2014
TEGETE AAMBIWA ARUDI SHULE AU AHAME YANGA.
Do you like this story?
Jerry Tegete |
BABA mzazi wa straika wa Yanga Jerry Tegete,
John Tegete amemtaka mwanae achague mawili ifikapo mwisho wa msimu huu iwapo
ataendelea kusugua benchi kwenye kikosi hicho.
Kocha huyo wa zamani wa Toto African ya
Mwanza alisema kuwa mbali na ukocha yeye pia ni mzazi hivyo lazima afuatilie
maendeleo ya mwanae.; “Naona mwanangu hana bahati na Yanga, licha ya kucheza
michezo minne na kufunga mabao matano. Naamini bado anaweza kucheza na
kupachika mabao, lakini kama hana nafasi basi nampa hadi mwisho wa msimu aweze
kuamua kati ya kusoma au kucheza soka nje ya Yanga,” amesema.
Kama ni kurudi shule basi Jerry ni kati ya
wachezaji watakaokuwa na elimu zaidi kwenye soka la Tanzania kwani tayari ni
mhitimu wa kidato cha nne. Lakini amefunikwa kielimu na Reliants Lusajo
mwenye Digrii ya ugavi, Salum Telela anayesoma Digrii ya Biashara na Issa Ngao
naye anayesomea biashara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TEGETE AAMBIWA ARUDI SHULE AU AHAME YANGA.”
Post a Comment