Friday, December 18, 2015
YANGA YAMKABIDHI JEZI GARBA TAYARI KUANZA KAZI
Do you like this story?
Klabu ya Yanga leo imemtambulisha rasmi
mchezaji wao wa kimataifa kutoka Niger Issoufou Boubacar Garba baada
ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili
kuitumikia Yanga kuanzia sasa.
Garba amesajiliwa siku chache kabla ya
dirisha dogo kufungwa baada ya benchi la ufundi la Yanga kujiridhisha na
kiwango chake kufuatia majaribio ya muda mfupi aliyofanya kwenye kikosi hicho
chini ya kocha mkuu Hans van Pluijm.
Garba amesema kila kitu kinakwenda sawa na
amewaahidi mashabiki wa Yanga kwamba, atapambana kuhakikisha anafanya vizuri na
kuisaidia Yanga kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali.
“Najisikia furaha tangu nimefika Tanzania
kujiunga na Yanga, kila kitu kinakwenda sawa kuanzia kwa kocha, wacheaji pamoja
na mashabiki. Yanga ni timu kubwa najivunia kucheza hapa na nawaomba mashabiki
wasubiri kuona kutoka kwangu”, amesema Garba.
Amepewa jezi namba 14 ambayo kabla yake
ilikuwa inavaliwa na beki wa kulia Joseph Zutta aliyesajiliwa kutoka Ghana
lakini mkataba wake na klabu hiyo ulivunjwa kwa kile kilichodaiwa ni kushindwa
kuonesha kiwango kilichotarajiwa na benchi la ufundi.
Mchezaji mwingine ambaye amesajiliwa na Yanga
katika kipindi cha dirisha dogo la usajili ni Paul Nonga ambaye hakuwepo wakati
wa utambulisho kutokana na kurejea kwenye klabu yake ya amani ya Mwadui FC ya
Shinyanga kwa ajili ya kuagana na timu hiyo na kufanya taratibu za kuhamia
jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “YANGA YAMKABIDHI JEZI GARBA TAYARI KUANZA KAZI”
Post a Comment