Thursday, December 17, 2015
MBEYA CITY WAENDELEA NA MAZOEZI KUKABILIANA NA MGAMBO JKT.
Do you like this story?
Na Mwandishi Wetu,
Mbeya
Kocha mkuu wa Mbeya
City FC 'Wanakoma kumwanya', Meja Mstaafu Abdul Mingange anaendelea na program
zake za mazoezi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa tayari kwa mchezo
ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Mgambo JKT uliopangwa kuchezwa
kwenye uwanja huo jumapili ijayo.
Kocha Mingange amesema
kuwa baada ya kumalizika kwa mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar
aliandaa mpango maalum ili kuwaweka fit wachezaji wake na anaamini mechi
itakuwa ngumu kutokana na matokeo ya sare waliyopata wapinzani wake katika
mchezo wao uliopita.
“Nina program maalumu kuhakikisha tunapata matokeo dhidi ya
Mgambo, najua kuwa walipata sare dhidi ya Yanga mchezo wao uliopita, hii ina
maana kuwa walitumia nguvu nyingi dhidi ya timu hiyo kubwa, ndiyo sababu
tunafanya aina hii ya mazoezi ya mbinu ili tuwe na uhakika wa matokeo” alisema.
Katika hatua nyingine
katibu mkuu wa City, Emmanuel Kimbe ameweka wazi kuwa usajili wa nyota wanne
uliofanywa mapema baada ya dirisha dogo kufungwa ndiyo pekee uliofunga kipindi
hiki cha usajili mdogo huku wachezaji wawili, Medson Mwakatundu na Rajabu seif
wakiwa wamepelekwa kwa mkopo kwenye tmu ya Geita Gold ya Geita.
“Abdallah Juma,Deo Julius,Ditram Nchimbi na Tumba Sued Lui ndiyo
wachezaji wapya kwenye kikosi chetu katika kipindi hiki cha dirisha dogo,huku
Medson Mwakatundu na Rajab Seif wakiwa wamepelekwa kwa mkopo Geita
Gold,hiyo ndiyo kauli pekee naweza kusema katika kipindi hiki” alisema katibu
Kimbe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “MBEYA CITY WAENDELEA NA MAZOEZI KUKABILIANA NA MGAMBO JKT.”
Post a Comment