Friday, December 18, 2015
NAULI KUPANDA MBEYA SUMATRA YATOA KAULI NZITO
Do you like this story?
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu nchni
SUMATRA Mkoa wa Mbeya imewatahadharisha wamiliki wa vyombo vya usafiri
kutokupandisha nauli katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho mwa
mwaka.
Afisa Mfawidhi wa SUMATRA mkoani Mbeya Denis Daudi amesema
mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua watoa huduma wakiwemo wamiliki,
wafanyakazi na wapiga debe wa vyombo vya usafiri watakaokiuka agizo hilo.
Akizungumza Denis amesema yamejengeka mazoea ya kila
inapofikia mwishoni mwa mwaka Mawakala wa kukatisha tiketi katika maeneo ya
vituo vya maabasi, wamiliki, madereva na makondakta kulalamikiwa na abiria kwa
tabia hiyo ambayo wanaifanya kwa lengo la kujiongezea kipato huku wakifahamu
kuwa ni kinyume cha sheria
SUMATRA imewataka abiria kuipa ushirikiano kwa kukataa
kulipa nauli isiyoendana na hadhi ya gari na umbali wa safari husika kwa kutoa
taarifa kwa Mamlaka hiyo ama kwa Askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama
barabarani.
Kutokana na wingi wa abira katika kipindi hiki SUMATRA pia
imewaruhusu wenye magari yanayoweza kusafirisha abiria kuyaombea kibali ili
yatoe huduma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ NAULI KUPANDA MBEYA SUMATRA YATOA KAULI NZITO”
Post a Comment