Friday, December 18, 2015
WANYARWANDA WASHIRIKI KURA YA MAONI
Do you like this story?
![]() |
| Rais Paul Kagame |
![]() |
| Wapiga kura 6 milioni wanatarajiwa kupiga kura |
Raia wa Rwanda
wameanza kufika vituoni kushiriki kwenye kura ya maoni ya marekebisho ya
katiba, ambayo yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa
muhula wa tatu.
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa asubuhi
na mapema, huku watu 6 milioni wakitarajiwa kupiga kura. Bw Kagame anatarajiwa
kupiga kura katika kituo cha Rugunga mjini Kigali.
Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda
yakamuwezesha Bw Kagame kusalia madarakani hadi 2034.
Marekani imetoa wito kwa Bw Kagame kuonyesha
uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017.
Lakini kiongozi huyo ameyashambulia mataifa
yanayotoa wito huo, akisema yanaingilia maswala ya ndani ya taifa hilo la
Afrika Mashariki.
Mwezi uliopita, Bunge la Seneti nchini Rwanda
liliidhinisha marekebisho hayo na kupisha kuandaliwa kwa kura ya maoni.
Bw Kagame atakuwa radhi kuwania urais kwa
muhula mwingine wa miaka 2017 marekebisho yakiidhinishwa.
Hata ingawa marekebisho hayo yanapunguza muda
wa muhula wa rais kutoka miaka saba hadi miaka mitano, na kudumisha muda wa
mihula miwili, sheria hiyo haitaanza kutekelezwa hadi mwaka 2024.
Hii ina maana Bw Kagame atakuwa huru kuwania
urais kwa mihula mingine miwili ya miaka mitano mitano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “ WANYARWANDA WASHIRIKI KURA YA MAONI”
Post a Comment