Thursday, April 10, 2014

AFISA MASOKO WA KAMPUNI YA COCA COLA AUAWA KWA KUMIMINIWA RISASI YA KIFUA MKOANI IRINGA.




NA FRANK KIBIKI, IRINGA
WATU wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi, kifuani Afisa masoko wa kampuni ya Vinywaji ya Coca-Cola Mkoani Iringa, Steven Mbwilo (40).

Kaim Kamanda wa Jeshi hilo, mkoani Iringa Wakyo Nyigesa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Pascal Benedict (44), mkazi wa Tunduma na Selemani Juma (42) mkazi wa Soweto mkoani Mbeya.

Alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi, saa sita mchana katika kijiji cha Mtiri, kata ya Ifwagi, Wilayani Mufindi ambapo watu hao walimvamia afisa huyo na kumpiga risasi iliyosababisha kifo chake papo hapo.
Hata hivyo, walisema kuwa marehemu huyo baada ya kupekuliwa alikutwa na fedha Shilingi Milioni 4.7 sambamba na simu yake ya mkononi.

Aliongeza kuwa sababu za mauaji hayo hazijajulikana na kwamba, uchunguzi zaidi unaendelea ili watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani kujibu shtaka linalowakabili.

0 Responses to “AFISA MASOKO WA KAMPUNI YA COCA COLA AUAWA KWA KUMIMINIWA RISASI YA KIFUA MKOANI IRINGA.”

Post a Comment

More to Read