Monday, April 14, 2014
AFUNGWA JELA MIAKA 15 KWA KUMUAMBUKIZA MWANAMKE VIRUSI VYA UKIMWI KWA MAKUSUDI .
Do you like this story?
MWANAMUME mwenye umri wa makamo,
Jumatatu alisukumwa jela kwa miaka 15, kwa kumwambukiza mwanamke Ukimwi maksudi
wakifanya mapenzi.
Hakimu Mkazi wa Iten, Bi Rose Ndombi,
alimpa Gilbert Kiptoo Barbos adhabu hiyo baada ya kumpata na hatia ya kufanya
mapenzi na mwanamke huyo akijua kwamba alikuwa na ukimwi.
Barbos alipatikana na hatia ya kufanya
mapenzi na mwanamke huyo mnamo Septemba 2, 2013, katika lojingi moja mjini Iten
Kenya, akijua wazi kwamba alikuwa na virusi vya ukimwi.
Mahakama iliambiwa kwamba alifanya
makosa hayo maksudi kwa kukosa kutumia kinga wakati wa kitendo hicho akijua
kwamba hatua hiyo, ingemfanya mwanamke huyo aambukizwe ukimwi.
Mbali na kosa hilo, Barbos alikabiliwa
na mashtaka mengine mawili ya ubakaji na wizi. Mahakama iliambiwa kwamba
aliiba simu aina ya Techno ya mwanamke huyo yenye thamani ya Sh3000 na Sh1000
pesa taslimu.
Mwendesha mashtaka, Bw Tom
Chitira aliambia mahakama kwamba Barbos, na mshukiwa mwingine ambaye hakuwa
mahakamani, walimwambia mlalamishi kwamba wangemsaidia kupata kazi mjini Iten.
Walipofika mjini Iten, Barbos alimpeleka mwanamke huyo katika lojing’i ambako
wangelala kabla ya kumpeleka kwa mtu ambaye alidai angemwajiri.
Mlalamishi aliambia mahakama kwamba
Barbos alimhandaa kwamba wangelala vyumba tofauti.
“Nafikiri alinilewesha kabla ya
kunipeleka katika lojing’i kwa sababu nakumbuka nikikataa pendekezo lake la
kulala chumba kimoja na mtu mgeni kwangu kabla ya kujipata katika chumba
alichokuwa siku iliyofuata,” mwanamke huyo aliambia mahakama. Alisema alipiga
ripoti katika kituo cha polisi cha Iten na mshtakiwa akasakwa na kukamatwa.
Maafisa wa polisi walimshauri mwanamke
huyo aende kupimwa baada ya kupata dawa za kuzima makali ya ukimwi (ARVs)
walipomkamata Barbos.
Ripoti ya daktari iliyowasilishwa
mahakamani ilionyesha kwamba baada ya kupimwa, iligunduliwa mlalamishi alikuwa
ameambukizwa virusi vya ukimwi.
Ubakaji
Hata hivyo, Bi Ndombi hakumpata
Barbos na hatia ya ubakaji akisema upande wa mashtaka haukuthibitisha shtaka
hilo kulingana na viwango vinavyohitajika kisheria, lakini akampata na hatia ya
kuambukiza mwanamke huyo ukimwi na kumuibia.
Akimhukumu, Bi Ndombi alisema Barbos
atafungwa jela miaka 15 ili kuwa funzo kwa wengine wanaofanya makosa kama hayo.
Alisema kwamba sheria iko wazi kwa wanaoambukiza wengine ukimwi maksudi.
Alimhukumu mshtakiwa kufungwa jela
miezi sita kwa kosa la wizi na akaagiza kila hukumu itekelezwe baada ya
nyingine. Alimpatia mshtakiwa siku 14 za kukata rufaa asiporidhika na hukumu
hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ AFUNGWA JELA MIAKA 15 KWA KUMUAMBUKIZA MWANAMKE VIRUSI VYA UKIMWI KWA MAKUSUDI .”
Post a Comment