Wednesday, April 16, 2014

AZAM WAJIBU MASHAMBULIZI KUHUSU KUNUNUA UBINGWA.




Zikiwa zimepita takribani siku nne tangu Azam FC ilipoandika historia ya bingwa wa mpya wa ligi kuu ya Vodacom huku tetesi zikizidi kuzunguka mitaani kwamba klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam imekuwa ikihonga sana wachezaji wa timu nyingine pamoja na marefa ili kujihakikishia ushindi na hatimaye kutwaa ubingwa kabisa.

Leo hii kupitia ukurasa wa wa Facebook, Azam FC wameposti taarifa ya kujibu mashambulizi dhidi yao kwamba wamenunua ubingwa kwa kuandika:

“Maneno yanayozungumzwa ni porojo Baada ya Azam Fc kupata mafanikio ya kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam Fc ilipata nafasi ya pili mara Mbili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara haikuwai kusemwa imenunua leo iweje imekuwa Bingwa isemwe imenunua.

John Bocco ameweka Historia Baada ya Kufunga Goli la Ushindi ktk Mechi ya Mwisho ya Ligi Daraja la kwanza na Kuipandisha Azam Fc kucheza Ligi kuu ya Tanzania Bara, na leo Hii Tumeshuhudia John Bocco ameweka Historia ya Kufunga Goli la Ushindi na Kuipa Timu ya Azam Fc Ubingwa kwa Mara ya kwanza Tangu ilipopanda Daraja kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara kwa Msimu 2013/2014 na kucheza Bila kupoteza hata mechi Moja.

Hatuto puuzia mechi ya mwisho Dhidi ya JKT Ruvu Tutacheza kama mechi nyingine Tulivyocheza Tunahitaji kuweka Historia ya Kutokupoteza hata Mechi Moja kwa Msimu Huu JKT Ruvu wajiandae kwa Kichapo wakati Tukiwa Tunakabidhiwa Kombe letu la Msimu Huu

Baadhi ya Maneno ambayo Makocha wanazungumza Sio Mazuri wao kama wataalam hawatakiwi kujihusisha katika Propaganda ambazo baadhi ya watu wanaziendeleza.”

0 Responses to “AZAM WAJIBU MASHAMBULIZI KUHUSU KUNUNUA UBINGWA.”

Post a Comment

More to Read