Wednesday, April 9, 2014
DEMBA BA AINUA CHELSEA.
Do you like this story?
Bao la dakika za lala salama za
mchezaji wa akiba Demba Ba ilitosha kuifikisha Chelsea katika hatu ya nusu
fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya Chelsea ilipoilaza Paris St-Germain
katika mechi ya marudiano
iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge Uingereza.
Bao hilo lilitibua shangwe kutoka
kwa kocha Jose Mourinho.
Chelsea ilikuwa imelazwa mabao 3-1
na PSG katika mkondo wa kwanza na ilikuwa hainabudi kufunga mabao 2-0
ilikufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya mchuano
huo
wenye kitita kikubwa zaidi barani.
Hata hivyo mechi hiyo ilivyoanza kwa
msisismko mkubwa ilisababisha kujeruhiwa kwa Eden Hazard mapema kunako dakika
ya 17 ya mechi hiyo.
Mourinho alimchezesha Andre Schurrle
ambaye hakukawia kabla ya kufunga bao la kwanza na kufufua matumaini ya the
Blues kutinga nusu fainali.
Mourinho, alitimuka mbio nje ya
uwanja na kukatiza sherehe ya wachezaji wake waliokuwa wakimshangilia Ba na
kuwahimiza wamakinike ilikuhakikisha wanafuzu kwa mkondo ujao sawia na hali
ilivyokuwa mwaka wa 2004 Porto
ilipoilaza Manchester United Old Trafford
Kocha wa PSG Laurent Blanc,alisalia kinywa
wazi asijue kilichotokea Stamford Bridge kwani hata mchezaji wa kutegemewa
Edinson Cavani hakuweza kuongoza kikamilifu mashambulizi baada ya mchezaji
wao wa kutegemewa Zlatan Ibrahimovic kukosa
kucheza mechi hiyo.
Kwa ''the special one'' hii itakuwa ni mechi
yake ya tatu ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Uropa akiwa mkufunzi
wa Chelsea japo alishindwa katika fursa zake za kwanza mbili na Liverpool.
Chelsea sasa wamefuzu kwa pamoja na Real
Madrid iliyoshindwa na Borussia Dortmund 2-0.
Real iliyokuwa ikicheza bila ya nyota wake
Christiano Ronaldo ilishinda mkondo wa kwanza 3-0.
Droo ya nusu fainali itafanyika ijumaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DEMBA BA AINUA CHELSEA.”
Post a Comment