Wednesday, April 9, 2014
NDEGE ILIYOTENGENEZWA NA HUYU MKENYA UMEIONA?ANATAKA KUIPAISHA.
Do you like this story?
Nchini Kenya kuna Mwanafunzi wa chuo kikuu
cha Naivasha ambae katengeneza ‘Ndege’ yake ambayo toka ameanza kuiunda alisema
lazima ipae huku akiwa katumia vifaa mbalimbali kutoka kwenye Bajaji kuiunda.
Mzigo ulipokamilika nyumbani kwao
alipoitengenezea, Polisi wa mji huo wakamkataza kuipaisha kwa sababu ni kinyume
na sheria lakini ili kuepuka kumkatisha tamaa… wakamwambia ni vyema akapata
kibali kutoka kwa mamlaka ya anga.
Paul Karanja alizuiwa na polisi kuipaisha hii
ndege kutoka uwanja wa mdogo wa ndege wa Karagita na kuwanyima uhondo zaidi ya
watu 500 waliofika asubuhi ya saa 3 kuangalia chombo kikipaishwa.
Hata hivyo Mwanachuo huyu wa chuo kikuu cha
Meru ana imani ataipaisha ndege yake siku moja ili kutimiza ndoto yake ambayo
hata hivyo ilipata hitilafu kwenye uwanja wa ndege wa Karagita kutokana na hali
mbaya ya uwanja huu iliyosababisha tairi la ndege yake kuharibika.
Karanja ambae ni Mwalimu pia wa shule ya
upili, amesema tayari ameiandikia barua mamlaka ya ndege nchini Kenya kuhusu
kupaisha ndege hiyo lakini hajapata majibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NDEGE ILIYOTENGENEZWA NA HUYU MKENYA UMEIONA?ANATAKA KUIPAISHA.”
Post a Comment