Thursday, February 27, 2014

WANANCHI WA MBEYA WAELEZA HISIA ZAO BAADA YA MCHEZAJI WA MBEYA CITY KUITWA KWENYE KIKOSI CHA TAIFA


KIKOSI CHA MBEYA CITY

BAADHI YA MASHABIKI WA MBEYA CITY



Na David Nyembe

Wakazi wa jiji la mbeya na vitogoji vyake wameeleza na kufuraishwa kwao na hatua ya kocha mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars) kuchukua mmoja ya wachezaji wa Mbeya City Fc Hassan Mwasapili ambayo inashiriki Ligi kuu Tanzania Bara.

Wakizungumza jijini Mbeya wakazi hao wamesema hatua hiyo inaleta chachu kwa vijana kuendelea kupenda mpira kwakuona ndio sehemu pekee ya kujiajiri wenyewe na kujipatia kipato badala ya kusubiri kuajiriwa.

Mmoja wa wakazi hao Bi Silivia Tawete mkazi wa soko matola amesema kuwa kwa muda mrefu Mpira ulikuwa haupendwi lkn kwa sasa ndio kimbilio kwa vijana wengi.

Kwaupande wake msemaji wa timu ya Mbeya City Bw Fredy Jackson ameonesha kufurahishwa na uteuzi huo huku akiamini kwamba umeleta hamasa kwa wachezaji wengine wa Mbeya City na mashabiki wake kwani mchezaji huyo hawakilishi Mbeya tu Bali ni taifa zima.

Hata hivyo amesema kuwa hatua hiyo itaendelea kuinua hali na nguvu na kuwapa hamasa wachezaji hao kuendelea kufanya vyema katika timu yao hatimaye waweze kufikia malengo yao.

Naye Mkazi wa eneo la Uhindini jijini mbeya Bwana Innocent John amedai kuwa hatua ya kocha kushuka chini na kuchukua wachezaji kwenye timu nyingine kunaonyesha wazi kuwa soka la Tanzania linaendelea kukua kwa kasi kwani awali ilizoereka kuwa wachezaji shiriki kwenye timu ya Taifa ni Simba na Yanga pekee hivyo hatua hiyo ni nzuri.





0 Responses to “WANANCHI WA MBEYA WAELEZA HISIA ZAO BAADA YA MCHEZAJI WA MBEYA CITY KUITWA KWENYE KIKOSI CHA TAIFA”

Post a Comment

More to Read