Na David Nyembe, Mbeya.
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, leo limemkabidhi Soko jipya la Kisasa la Mwanjelwa mkandarasi mpya kutoka Kampuni ya Nandhra Engineering & Construction Company baada
ya mkandarasi wa awali kuvunja mkataba.
Kuvunja kwa mkataba huo, kumetokana na Mkandarasi huyo kutoka Kampuni ya Tanzania Bulding Works
Limitted ya Jijini Dar es Salaam, kushindwa
kukamilisha ujenzi wa soko hilo kwa
wakati kwani Julai 2012 soko hilo lilipaswa kukamilika na
kukabidhiwa kwa uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya,
Mussa Mapunda, amesema mkandarasi huyo mpaya atatuumia shilingi
bilioni 5.0 katika kukamilisha ujenzi wa soko hilo ambao mpaka sasa umetumia
zaidi ya shilingi Bilioni 11 kati ya
Bilioni 13 .
Amesema, katika kiasi hicho cha
fedha cha shilingi bilioni 13 kiasi kilichobakia ni shilingi Bilioni 1.8 hivyo
kuilazimu halmashauri hiyo kukopa tena kiasi cha fedha cha shilingi Bilioni 3.5 kutoka Benki ya CRDB kwa
ajili ya kumalizia ujenzi huo.
Akikabidhiwa
ujenzi wa Soko hilo Mkandarasi Kulwant Singh aliwahahidi wakazi wa Jiji la
mbeya na uongozi kwa ujumla kuwa atahakikisha kazi hiyo itakamilika katika
kipindi walichoandikiana kwenye mkataba hivyo serikali kuondoa mashaka.
Ujenzi huo unadaiwa kusimama
kwa zaidi ya miezi saba tangu Mkandarasi wa awali asitishe
mkataba wake na kwamba ujenzi huo unatarajia kuanza Aprili mwaka huu na kukabidhi soko hilo Desemba mwaka huu
Soko la
Mwanjelwa liliteketea kwa moto mwaka 2006 na kusababisha hasara ya mamilioni ya
fedha kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya 2000 walionguliwa maduka yao.
|
0 Responses to “JIJI LA MBEYA LAPATA MKANDARASI MPYA SOKO LA MWANJELWA”
Post a Comment