Wednesday, February 26, 2014

SIRI YA UFAULU WA ST FRANCES MBEYA


UBAO WA MATANGAZO KATIKA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA ST FRANCIS 

MMOJA WA WAALIMU WA ST FRANCES AKITOA MAELEZO

MMOJA YA MAJENGO YA SHULE HIYO YANAYOTUMIKA KUTOLEA ELIMU


Na David Nyembe,Mbeya
 
Ubora wa Mazingira katika shule ya  Shule ya Sekondari ya St.Francis ya Jijini Mbeya, Tanzania, wametajwa kuwa chachu ya mafanikio ya shule hiyo.
 
Moja ya vitu muhimu vinavyo fanya shule hiyo kuwa bora ni pamoja na suala la upatikanaji wa chakula bora cha kuwajenga wanafunzi pamoja na upatikanaji wa vifaa muhimu vya kufundishia.
 
 
Hata hivyo Uongozi huo umedai kuwa ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri katika mitihani na kuendelea katika elimu ya juu anapaswa kuzingatia mambo ya msingi ya: kimaadili, kuipenda shule na kuwapenda na kuwaheshimu walimu na kuamini kuwa ni sehemu ya wazazi wao katika malezi.
 
 
Akizungumza jijini mbeya   Mkuu wa shule hiyo Sista Flossy Sequira Amesema siri kubwa katika mafanikio ya shule hiyo ni kumtanguliza mungu kwanza pamoja na kila mmoja katika shule hiyo  kuanzia na uongozi hadi  walimu kutambua wajibu wao wa kazi.
 
Hata hivyo amedai kuwa mambo mengine  ni kuangalia lengo la msingi lililowafikisha shule, mpango mikakati ya kufikia lengo ikiwemo na mbinu za kuondokana ama kutatua vikwazo vitakavyojitokeza shuleni hapo .
.
 
 
Amesema suala la  nidhamu kuwa ni chanzo na ufunguo wa ufahamu katika elimu kwani wao wanaamini walimu ni wazazi wao kama waliowaacha nyumbani, uwajibikaji kila mahali, kusali kwa pamoja bila kujali itikadi za dini, kupenda masomo yote kuanzia hisabati sanjari na kushiriki michezo mbalimbali.
 
 
K wa upande wake Mmoja wa walimu wa shule hiyo Ndugu Erasto Batholomeo ambaye ni mwalimu wa Hisabati amesema  kuwa endapo wataona mwenzao yupo nyuma katika masomo wanamuunganisha na mwanafunzi anayefanya vizuri katika darasa husika na kumpatia maswali hadi anafikia kiwango cha daraja la A kama ilivyo lengo lao kwa wanafunzi wote, kwa mujibu wa taratibu za uongozi wa shule.
 
 
 Amesema sifa ya mafaniko mengine kwa mwanafuzni wa shule hiyo kufanya vizuri ni kutokana na uwepo wa mazingira mazuri ya kujisomea  pamoja na  upatikananji wa chakula bora ambacho humjenga mwanafuzni kiulewa zaidi mara  awapo darasani .

0 Responses to “SIRI YA UFAULU WA ST FRANCES MBEYA”

Post a Comment

More to Read