Tuesday, February 25, 2014

54 WAKAMATWA KWA UNYWAJI WA POMBE SAA ZA KAZI JIJINI MBEYA


Mfanyabiashara wa pombe za kienyeji akiwa katika harakati za kuuza majira ya saa tatu asubuhi

Vibanda vinavyotumika kwaajiri ya pombe za kienyeji


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahamed MsangiM


Na David Nyembe, Mbeya.

LICHA ya Polisi Mkoani Mbeya, kufanikiwa kukamata watu 54 kwa unywaji wa pombe saa za kazi, wakazi wa Jiji la Mbeya  wameliomba jeshi hilo kuvifungia vialabu vya pombe na kumbi za starehe ambazo zitabainika kuendesha shughuli hizo nyakati za kazi.

Wakitoa kero hizo leo kwa mwakilishi wa Fahari News, baadhi ya  wakazi wa eneo la Mabatini, wamesema mwaka 2009 serikali kupitia sheria ndogo za halmashauri ilifanikiwa kutekeleza zoezi hilo kwa kudhibiti unywaji wa pombe saa za kazi kwa kuvifungia vilabu vya pombe, kumbi za starehe na mchezo wa Pool Table.

Wamesema zoezi hilo  lilifanikiwa kwa asilimia 100 kwani mwananchi aliyebainika kukiuka sheria hiyo aliwajibika kwa kulipa faini ya shilingi 50,000/= na wale walioshindwa walifikishwa mahakamani.

“Unajua ndugu mwandishi vijana wetu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwa unywaji wa pombe, kuendekeza anasa kwenye kumbi za starehe pamoja na kucheza mchezo wa pool table badala ya kufanya kazi mashambani,”amesema Joseph Mwakambili mkazi wa Mabatini

Amesema, vijana wengi wamekuwa wakikimbia kazi mashambani huku wakitambua njia pekee ya kuondokana na hali ya umaskini ni kujikita zaidi kwenye  sekta ya kilimo na mifugo  kwani ndio nguzo pekee itakayowatoa kwenye dimbwi la umaskini.

Mapema mwaka huu Polisi Mkoani Mbeya, kupitia zoezi la  ukamati wa watu ambao wanajihusisha na vitendo vya unywaji wa pombe saa za kazi limefanikiwa kukamata watu  54.

Kaimu Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Mbeya Robert Mayala, amesema watu hao walikamatwa katika matukio mawili tofauti ambapo    February 24 mwaka huu saa sita za mchana katika Mtaa wa Ilemi  walikamatwa watu 17 huku January 22 mwaka huu walikamatwa watu 37 Jijini Mbeya.

Hata hivyo, Mayala amewataka wakazi wa Mbeya kuheshimu na nidhamu katika muda wa kazi si muda  na kwamba si muda wote wakausudisha pombe na kuendekeza starehe ambazo hazimsaidii mtu kuondokana na hali ya umaskini.

Mwisho.

0 Responses to “54 WAKAMATWA KWA UNYWAJI WA POMBE SAA ZA KAZI JIJINI MBEYA”

Post a Comment

More to Read