Wednesday, April 9, 2014

AJALI ZA BARABARANI ZAONGEZEKA KWA KASI MKOANI IRINGA.




TAKWIMU zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la ajali za barabarani mara saba zaidi zinazohusisha pikipiki Mkoa wa Iringa kati ya Januari 1 hadi Machi 31 ikilinganishwa na miezi kama hii mwaka jana.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Iringa, Leopold Fungu, alisema ongezeko la ajali hizo linasababishwa na biashara ya pikipiki kubeba abiria.

Alisema jumla ya ajali zote za pikipiki kipindi hicho kwa mwaka huu ni 19 ikilinganishwa na ajali 12 za mwaka jana kwa kipindi kama hicho.

Kuhusu vifo vinavyotokana na ajali hizo, alisema vimeongezeka hadi kufikia 12 kwa mwaka huu   ikilinganishwa na mwaka jana ambapo vilitokea vifo 8 sawa na ongezeka la vifo vinne kwa ajali za pikipiki.

Kamanda Fungu alisema ajali hizo zilisababisha majeruhi ambapo kwa kipindi hicho watu saba walijeruhiwa tofauti na mwaka jana ambapo waliojeruhiwa walikuwa watatu wakati mwaka huu walikuwa wanne.

Aliwataka madereva wa pikipiki kuzingatia sheria zilizowekwa ili kupunguza ajali zinazosababisha hasara kwa familia na taifa.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, ongezeko la ajali hizo limesababisha polisi kuweka mikakati ya kuzipunguza kwa kipindi kilichobaki cha mwaka 2014 ambapo ni ushiriki wa jamii na elimu kwa umma na kwamba watapanua wigo wa kueneza elimu kwa umma.

Na Denis Mlowe, Iringa

0 Responses to “AJALI ZA BARABARANI ZAONGEZEKA KWA KASI MKOANI IRINGA. ”

Post a Comment

More to Read