Tuesday, January 19, 2016
TRA YATANGAZA TAREHE YA MWISHO YA KUBADILISHA NAMBA ZA PIKIPIKI MKOANI MBEYA
Do you like this story?
SERIKALI,
kupitia mamlaka ya mapato, (TRA),mkoani hapa imesema kuwa zoezi la kubadilisha
namba za usajili wa pikipiki kutoka T, kwenda MC, litamalizika mwishoni mwa
mwezi huu.
Kaimu Meneja wa mamlaka ya mapato, mkoani hapa Lukasi Mnabi alisema juzi kuwa zoezi hilo linahusu pikipiki za kawaida maarufu kama bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu (bajaji).
Amesema serikali imeamua kuongeza muda wa siku thelathini kuanzia januari mosi hadi januari 31 ili kuhakikisha kuwa madereva wa vyombo hivyo wawe wamevisajili kwenye usajili wa MC.
Amesema awali zoezi hilo lilitakiwa kumalizika Disemba 31, mwaka jana lakini kutokana na wingi wa vyombo hivyo serikali iliona umuhimu wa kuongeza siku 30, ili kutoa fursa kwa wote kusajiliwa.
“Kwa sababu tayari serikali imeongeza siku thelathini nina imani watu watakuja kusajili vyombo vyao baada ya hapo hatutaraji kuongeza muda zaidi, kitakachofuata ni kuwakamata na kuwachukulia hatua wale ambao watakuwa bado” amesema.
Amesema kuwa TRA, kwa kushirikiana na jeshi la polisi itafanya oparesheni maalum ya kukagua pikipiki ambazo hazitasajiliwa kwenye mfumo mpya mara baada ya muda uliowekwa kumalizika.
Amesema serikali iliamua kufanya hivyo baada ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali kwenye vyombo hivyo ikiwemo kutotambua aina ya pikipiki ya mtu binafsi na biashara.
Nao baadhi ya madereva wa bodada jijini Mbeya akiwemo Anord Abrahamu na Michael Mwalusamba wameungana na serikali kwa kuwataka wenzao ambao hawajasajili vyombo vyao kusajili kabla ya muda kuisha.
“Ni uzembe tu kwa baadhi ya madereva na wamiliki wa pikipiki serikali ilitangaza muda mrefu tangu mwaka juzi na ilitakiwa iwe mwisho mwaka jana mwezi wa kumi na mbili lakini kwa muda huo mtu anakuwa bado hajasajili mimi naona serikali iwachukulie hatua za kisheria” amesema Michael Mwalusamba.
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRA YATANGAZA TAREHE YA MWISHO YA KUBADILISHA NAMBA ZA PIKIPIKI MKOANI MBEYA”
Post a Comment