Monday, January 18, 2016
KIWANDA CHA SUKARI CHA MTIBWA CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 50 KWA KUKIUKA SHERIA ZA MAZINGIRA.
Do you like this story?
Serikali imetoa siku saba kwa kiwanda cha sukari cha Mtibwa
kulipa faini ya shilingi milioni 50 baada ya kudaiwa kukiuka sheria za
mazingira.
Baadhiya mambo yaliyobainika ni kukosa mfumo mzuri wa
kuhifadhi na kusafirisha taka ngumu na taka maji, kutohifadhi vyema kemikali
zinazotumiwa na kiwanda hicho pamoja na kutumia kuni kuendesha baadhi ya mitambo
yake hususani eneo la kuchemshia.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanywa kwa ziara ya
kushtukiza kiwandani hapo na naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais
muungano na mazingira Luhaga Mpina, aliyeambatana na wataalamu kutoka baraza la
taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC).
Mh Mpina amesema tayari serikali ilishakataza viwanda
kutumia kuni na magogo kuendeshea mitambo yake, huku akitoa siku 30 kwa uongozi
wa kiwanda hicho cha Mtibwa kufanyia marekebisho mapungufu yote yaliyotajwa
vinginevyo serikali itakifunga.
Akiwa kiwandani hapo naibu waziri Mpina amewaagiza viongozi
wa mamlaka mbalimbali kuwajibika katika agizo la usafi wa mazingira kwa kila
Jumamosi ya mwisho wa mwezi sambamba na kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri za
wilaya kuhakikisha miti milioni 1.5 inapandwa kila mwaka.
Kaimu meneja mkuu wa kiwanda cha sukari Mtibwa Ahmad Yahya
pamoja na kuridhia maagizo yaliyotolewa, ameiomba serikali kuwapunguzia faini
hiyo ya shilingi milioni 50 ambayo amedai kuwa ni nyingi kwa kiwanda hicho
kumudu
Chanzo>>Fredynjejeblogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIWANDA CHA SUKARI CHA MTIBWA CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 50 KWA KUKIUKA SHERIA ZA MAZINGIRA. ”
Post a Comment