Friday, January 22, 2016

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZATANGAZWA




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametangaza kamati za Bunge na majina ya wabunge waliochaguliwa katika kamati hizo kwa mujibu wa sheria.

Sura za wabunge wa zamani zimechanganyika na sura mpya katika kamati hizo ambapo Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT) na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (CHADEMA) ni miongoni mwa wanaounda kamati ya huduma za maendeleo ya jamii.

Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM), Naghejwa Kaboyoka Same mashariki (CHADEMA)Livingstone Lusinde Mtera (CCM) wameteuliwa kujumuika katika kamati ya Hesabu za serikali PAC.

Kamati nyingine ni pamoja na Kamati ya Uongozozi ikiwa na Spika Job Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM), Freeman Mbowe Hai (CHADEMA) George Masaju ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengineo.

Kamati ya sheria ndogo waliopata nafasi ni pamoja na Halima Mdee Kawe (CHADEMA),Abdalah Mtolea Temeke (CUF) ,Tundu Lissu Singida Mashariki (CHADEMA),Ridhiwani Kikwete Chalinze (CCM).

Baadhi ya wanaounda kamati ya Serikali za mitaa ni pamoja na Kangi Lugola Mwibara (CCM) Leah Komanya Viti maalum (CCM) Saada Mkuya Welezo (CCM) na wengineo.

Aidha Spika wa Bunge amesema kuwa kamati hizo zimeundwa kwa kuzingatia uzoefu wa wabunge hao,taaluma zao na jinsi walivyojaza fomu za kuomba kamati hii
MAJINA YA KAMATIO ZOTE SOMA HAPA

0 Responses to “ KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZATANGAZWA ”

Post a Comment

More to Read