Saturday, April 12, 2014

HALI YA HEWA YA TUKUYU YAWATATIZA VIJANA WA MABORESHO WA TAIFA STARS.


Meneja wa Timu Ndugu Boniface Clemence akizunguzia juu ya maendeleo ya Kambi hiyo







Chuo cha Uwalimu Cha Msasani ambacho uwanja wake unatumika kwa vijana hao




KIKOSI cha Wachezaji 33 Cha timu ya maboresho ya Taifa Stars, kimeendelea vyema katika  kambi yake iliyoko Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani mbeya katika Hotel ya Land Mark Hotel.

Uwanja unaotumika na wachezaji hao kwa jaili ya mazoezi ni  katika Chuo Cha Ualimu Cha Msasani kilichopo hatua kadhaa toka katika Hotel hiyo.

Akizungumza na Blog hii Meneja wa Timu hiyo Ndugu Boniface Clemence amesema kuwa kambi ya vijana hao inaendelea vyema licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.

Amesema kwa asilimia kubwa vijana hao wapo katika afya njema hasa kutokana na kupatiwa huduma nzuri zilizopo kambini hapo.

Amesema vijana hao wameonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa kuonyesha ushirikiano kutoka kwa viongozi wao.

Hata hivyo Kocha Mkuu Ndugu Oscar Koloso amesema kuwa maendeleo ya vijana hao yako vizuri licha ya kukumbana na hali ya hewa yenye baridi kali hali ambayo imewafanya baadhi yao kuteteleka kidogo hasa kutokana na mazingira waliyotoka.

Amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kila siku hali ambayo inawafanya wafanye mazoezi na mvua hizo huku siku nyingine kulazimika kufanya mazoezi ya kukimbia tu badala ya kuimgia uwanjani.

Amesema kwa sasa wapo katika hatua ya kufanya mazoezi magumu ya kukimbia na mpira kwani mazoezi magumu ya viongo wamekwisha kamilisha.

Hata hivyo Kocha huyo amebainisha kuwa wamejaribu kwenda haraka hasa kutokana na muda kuwa mchache katika kambi hiyo ambayo kwa hatua ya kwanza wanatakiwa kukaa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Wachezaji waliobahatika kuingia kwenye mchakato huo wa maboresho ya Taifa Stars kuwa ni  Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi), Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga), Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri Ali (Kaskazini Unguja) ambao ni makipa.

Kwa upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba (Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).

Mabeki wa kati ni Abbas Ali Haji (Kaskazini Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma Namwamba (Temeke), Hussein Juma Akilimali (Njombe), Joram Nasson (Iringa), Kayombo Silvanus Henrico (Ilala), Miraji Maka (Mwanza),  Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini Unguja) na Said Juma Ali (Mjini Magharibi).

Viungo wapo Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga), Juma Said Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga), Ryna Mgonyike (Temeke) na Yusuf Mpilipili (Temeke).

Washambuliaji ni Abdallah Kagumbwa (Temeke), Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Athanas Fabian Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu (Mwanza), Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Chunga Said (Manyara), Mbwana Mshindo Mussa (Tanga), Michael David Mlekwa (Lindi), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar Athuman Nyenje (Mtwara), Paul Michael Bundala (Ilala), Ramadhan Kapalamoto (Kinondoni) na Roman Nyapunda (Temeke).

0 Responses to “HALI YA HEWA YA TUKUYU YAWATATIZA VIJANA WA MABORESHO WA TAIFA STARS.”

Post a Comment

More to Read