Saturday, April 12, 2014
KIJANA AFARIKI AKIJARIBU KUVUNJA REKODI YA DUNIA MCHEZO WA HATARI.
Do you like this story?
Roy akijaribu kujinasua kwa mikono baada ya kuwa amenasa nywele
zake.
Mchezaji michezo ya hatari amefariki
dunia katika harakati zake za kuweka rekodi ya dunia wakati akijaribu kuvuka
juu ya mto mmoja kwa kutumia waya mwembamba ulioungwa katika nywele zake.
Sailendra Nath Roy, miaka 50, alikuwa
nusu ya safari yake kupitia mkogo huo ndipo mtindo
wake wa nywele uliponasa kwenye kifundo cha waya aliokuwa akisererekea na
kubaki akining'inia angani kwa takribani dakika 25.
Licha ya majaribio kadhaa kujinasua
mwenyewe, inaaminika Roy kisha alipatwa na mshituko wa moyo na kufariki dunia.
Roy, mlinzi katika Jeshi la Polisi wa West Bengal, tayari
alikuwa akishikilia rekodi ya dunia ya Guinness kwa kusafiri umbali
mrefu zaidi kwenye waya mwembamba kwa kutumia nywele zake.
Takribani watu 1,000 walijitokeza
kwenda kumshuhudia akijaribu na kuvunja rekodi hiyo juu ya Mto Teesta mjini Darjeeling, ambao ni karibu
futi 10,000 juu ya usawa wa bahari, ndipo ajali hiyo isiyo ya kawaida
ilipotokea.
Roy alijaribu kujinasua mwenyewe baada
ya mtindo wake wa nywele kunaswa kwenye kifundo katika waya na kisha kujaribu
kuendelea kuvuka akitumia mikono yake pekee.
Hatahivyo, vyombo vya habari mjini humo
vilisema kisha baadaye akapatwa na mshituko wa moyo.
Waokoaji walimshusha chini kutoka
Daraja hilo la Kutawazwa takribani dakika 45 baadaye.
Alipelekwa katika hospitali ya karibu
lakini alithibitishwa kufariki wakati alipofikishwa hospitalini hapo.
Mashuhuda walisema washangiliaji
mwanzoni walishindwa kubaini Roy alikuwa kwenye matatizo sababu ya kelele
zilizokuwa zikitoka kwa umati huo.
Mchezaji huyo wa michezo ya hatari
amewahi kushikilia rekodi kadhaa za Guinness duniani kwa kuvuta magari kwa
kutumia nywele zake.
Alivutia wengi duniani mwaka jana pale
alipokokota garimoshi lenye tani 42 kwa umbali wa mita 2.5.
Mwaka 2011, alisafiri umbali wa futi
270 juu ya waya mwembamba, ambao ulishikizwa kwenye nywele zake.
Kamishna wa Polisi wa Siliguri, K.
Jairaman alisema Roy hakutakiwa kupata ruhusa muhimu kwa ajili ya mchezo huo wa
hatari, akiongeza kwamba Roy hakuwa kazini wakati alipofikwa na mauti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIJANA AFARIKI AKIJARIBU KUVUNJA REKODI YA DUNIA MCHEZO WA HATARI.”
Post a Comment