Tuesday, April 22, 2014
HOT NEWSS ASKARI WA JESHI LA POLISI NA WENZIE WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA.
Do you like this story?
| Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali. |
| Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha |
| Ulinzi mkali uliimalishwa mahakamani hapo |
MAHAKAMA
ya Mkoa wa Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela waliokuwa askari wawili,
James Kagoma wa Jeshi la Polisi na Juma Mussa wa Jeshi la Magereza na raia
watatu, baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya Unyang’anyi wa Kutumia
Silaha.
Mbali na
kifungo hicho, mahakama hiyo pia imeamuru kutaifishwa kwa magari mawili madogo
yaliyotumika katika unyang;anyi huo, ambayo ni mali ya aliyekuwa askari Polisi,
James Kagoma na lingine la mshtakiwa namba mbili katika kesi hiyo, Elinaza
Mshana.
Akitoa
hukumu hiyo iliyochukua muda wa saa Mbili na dakika 30 kuanzia saa 4:20 asubuhi
hadi saa 6:30 mchana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya,
Michael Mteite, amesema upande wa mashtaka umefanikiwa kuitihibitishia mahakama
hiyo bila shaka kuwa washtakiwa wote watano wametenda kosa hilo Januari 3 mwaka
huu, saa 11 jioni kwenye mlima Kawetele barabara ya kutoka Mbeya kwenda
Chunya kwa kuwapora wafanyabiashara wawili wenye asili ya kiasia shilingi
milioni tatu na nusu na vitu mbalimbali zikiwemo simu mbili za mkononi, laptop
mbili na mabegi matatu ya nguo.
Mbali na
askari hao wa zamani, James Kagoma na Mussa Juma na raia Elinaza Mshana,
wengine waliohukumiwa kifungo hicho ni Mapacha, Mbaruku Hamisi na Amri
Kihenya, huku upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Achiles
Mulisa akisaidiwa na Basilius Namkambe na washtakiwa hao wakitetewa na Jopo
lililoongozwa na Wakili Ladislaus Rwekaza akisaidiwa na John Stephen na Daniel
Muya.
Hakimu
Mteite, amesema mahakama imefikia uamuzi huo kwa kuzingatia mambo Sita, Kwanza
ni kufananana kwa ushahidi wa uliotolewa na aliyekuwa dereva wa wafanyabiashara
hao, Ezekia Matatila na Mmoja kati wa Wafanyabiashara hao, Pasupuret
Sreedhar ambaye ni raia wa India.
Pili ni
kuwiana kwa ushahidi wa mashahidi hao na maelezo ya tukio hilo kutoka kwa
Maafisa Wanne wa Polisi waliotoa ushahidi wao mahakamani hapo ambao ndiyo
waliowakamata washtakiwa hao siku ya tukio.
Tatu ni
maelezo ya utetezi ya washtakiwa hao kuthibitisha kuwa siku ya tukio wote
walikuwa pamoja katika eneo la tukio na muda unaodaiwa kufanyika tukio hilo.
Nne ni
uthibitisho kuwa vitu vyote vinavyodaiwa kuporwa na washtakiwa hao kutoka kwa
Wafanyabiashara hao kukutwa kwenye magari mawili waliyokuwa wakiyatumia ambayo
ni Toyota Cresta namba T 782 BEU mali ya Elinaza Mshana na Grand Mark II
lenye namba za cheses GX 115 6011835 mali ya aliyekuwa askari Polisi,
James Kagoma.
Tano ni
jeraha la risasi la mshtakiwa namba mbili, Elinaza Mshana, kwenye paja lake la
mguu wa kulia, linathibitisha maelezo ya askari polisi kuwa walilazimika
kumpiga risasi ya mguu ili kumzuia asikimbie siku ya tukio hilo.
Na Sita,
Hakimu Mteite, amesema kitendo cha Shahidi wa Kwanza, dereva Ezekia Matatila na
Shahidi wa Tatu, Mmoja kati wa Wafanyabiashara walioporwa, Pasupuret Sreedhar,
kuwatambua kwa ufasaha washtakiwa hao mahakamani hapo.
Kutokana
na ushahidi huo, Hakimu Mteite, amesema mahakama yake imewahukumu washtakiwa
hao kifungo cha miaka 30 jela na kuamuru magari hayo mawili kutaifishwa huku
akiondoa adhabu ya kuchapwa viboko kwa sababu ya huruma kufuatia kupigwa risasi
kwa mshtakiwa namba mbili, Elinaza Mshana.
Hata
hivyo, Wakili Kiongozi wa Upande wa Utetezi, Ladislaus Rwekaza amesema
wanataraji kukata rufaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “HOT NEWSS ASKARI WA JESHI LA POLISI NA WENZIE WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA. ”
Post a Comment