Tuesday, April 22, 2014
KUIONA STARS, BURUNDI BUKU 5 TU!!.
Do you like this story?
Kiingilio
cha chini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa
ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa
Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Mechi
hiyo itakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, na kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya
chungwa, bluu na kijani. Kwa wa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000
wakati VIP B na C ni sh. 10,000.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini
kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka nchini Kenya.
Burundi
inatarajia kuwasili nchini keshokutwa (Aprili 22 mwaka huu) tayari kwa
ajili ya mechi hiyo inayotajiwa kuwa ya kusisimua. Mechi hiyo imepangwa
kuanza saa 10 jioni.
Wachezaji
wa Taifa Stars waliopo kambini ni Deogratias Munishi, Mwadili Ali,
Aidan Michael, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Hassan Mwasapili, Kelvin
Yondani, Said Moradi, Amri Kiemba, Frank Domayo, Himid Mao, Jonas Mkude,
Athanas Mdamu, Haruna Chanongo, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa,
Ramadhan Singano na Simon Msuva.
Wengine
ni Benedicto Mlekwa, Emma Simwanda, Joram Mgeveje, Omari Kindamba,
Edward Mayunga, Shiraz Sozigwa, Yusuf Mlipili, Said Ally, Abubakar
Mohamed, Hashim Magona, Omari Nyenje, Chunga Zito, Mohammed Saidi, Ayoub
Lipati, Abdurahman Ally na Paul Bundara.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUIONA STARS, BURUNDI BUKU 5 TU!!.”
Post a Comment