Thursday, April 17, 2014
MAWIMBI YATATIZA UOKOZI KOREA YA KUSINI.
Do you like this story?
Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa
baharini imetatiza juhudi za utafutaji na uokoaji wa takriban watu mia tatu
baada ya feri ya abiria kuzama katika pwani ya Korea Kusini.
Watu tisa wamethibitishwa kuaga
dunia katika mkasa huo.
Wengi wa abiria kwenye meli hiyo
walikuwa ni wanafunzi wa shule ya upili. Takriban watu mia moja sabini
wameokolewa. Kapteni wa jeshi la wanamaji la Marekani Heidi C. Agle anashiriki
katika operesheni ya uokoaji.
Ameiambia BBC kuwa maandalizi
yanafanywa kupeleka mtambo wa kuinua chombo hicho.
Wakati huohuo Rais Park Geun-hye,
amewataka waokozi kuharakisha juhudi zao za kuwatafuta manusura wa ajali hiyo.
Rais Park -- ambaye amejionea meli
hiyo mwenyewe, amesema kuwa kila dakika ni muhimu katika kuhakikisha kuwa
manusura wanapatikana.
Wapiga mbizi wamekuwa wakikabiliana
na mawimbi makali kujaribu kukifikia chombo hicho kilichozama hapo jana.
Duru zinasema kuwa meli hiyo
ilipoteza mwelekeo huku baadhi ya familia za waathriwa zikihoji mwenendo wa
nahodha wa meli.
Hata hivyo nahodha huyo Lee
Joon-seok aliomba msamaha na kusema ana majuto tele na kuwa hata hajui la
kusema.
Dauru zinseama kuwa miongoni mwa
wliofariki ni wanafunzi wanne wenye umri wa miaka 17 na mwaliamu wao mwenye
umri wa miaka 25 pamoja na mfnyakazi mmoja wa meli hiyo.
Wengine wlaiofariki bado
hawajatajwa.
Takwimu za hivi karibuni zinasema
kuwa wtu 475 walikuwa kwenye meli hiyo huku 287 wakiwa bado hawajapatikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAWIMBI YATATIZA UOKOZI KOREA YA KUSINI.”
Post a Comment