Thursday, April 17, 2014
MH LUKUVI AJIBU MAPIGO YA WAPINZANI BUNGENI KUHUSU KAULI YA JESHI KUTAWALA NCHI.
Do you like this story?
April 17 2014 Wajumbe walio upande wa
(UKAWA) kwenye bunge la katiba wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba waligoma
na kuamua kutoka nje ya bunge hili hapa Dodoma baada ya Profesa Lipumba
kumaliza kuzungumza kwamba hawawezi kuendelea na bunge la matusi na ubaguzi.
Kingine kikubwa alichozungumza Prof.
Lipumba ni kusikitishwa na kauli ya Waziri Lukuvi aliyoitoa kanisani weekend
iliyopita kwamba jeshi litatawala nchi ambapo April 14 2014 gazeti la Mwananchi
lilimnukuu Waziri Lukuvi akisema Kanisani ‘tukipitisha serikali tatu jeshi
litatawala nchi’
Kama hutoweza kusikiliza sauti yake
hapa chini yafuatayo ni baadhi ya makubwa aliyoyazungumza leo asubuhi
‘Ni kweli kwamba kikao hichi nilipanga
nisichangie kwa sababu niliona mechi kali tukishindilia watu watakufa,
sikusikia vizuri yaliyotokea jana ila mimi sio mnafiki, nampongeza sana Mh.
Mrema kwa hotuba yake juzi, Mrema ndio mpinzani wa kweli, alisema angalia mambo
yanayotokea Znz msidhani yataishia Magogoni’
‘Baada ya hotuba ya Rais, mh. Seif
Sharrif Hamad alihutubia, yeye ni mchochezi wa hovyo kwa kumsingizia Rais,
hakuna mtu yeyote anaweza kunizuia kusema ninayoyaamini mimi, sio hapa wala
mtaani, ni kweli Jumamosi nilimwakilisha Waziri mkuu ambae hakunipa hotuba na
mambo yalinoga nikatawazwa kuwa chifu’
‘Viongozi wa dini waliliombea Bunge
pale Kanisani, mimi Waziri nipo pale… nisiongee chochote??!! tukiendeleza
ambayo hayako kwenye mila zetu Znz na Tanganyika inaweza kuwa kama Korea
kaskazini na kusini, hofu niliyonayo ni juu ya rasimu yenyewe kwa sababu kwanza
imejengwa kwenye misingi ambayo siiamini’
‘Zanzibar inatambulika kama nchi kwenye
katiba yao toka hata kwenye katiba ya nyuma kabisa, yapo mapungufu muundo wa
serikali 3, ukisoma rasimu wanasema serikali ya Tanganyika imevaa koti la
muungano lakini koti lenyewe tunapokezana, leo anavaa Mwinyi, leo anavaa huyu’
‘Hatujawahi kutoa bajeti inayotosha kwa
jeshi la Wananchi, mmeshawahi ona wanaandamana kudai haki zao? nina miaka zaidi
ya 50 na nisingependa kuiona Tanzania hii inakwenda kwenye maisha ambayo
sikuyazoea ili kuepusha haya tusijaribu tusichokijua, hii ni hofu yangu… hakuna
wa kunizuia kutoa hofu yangu’
‘Ukweli ni kwamba kama umesoma hii
rasimu, muundo unaweza kuwa umeandikwa vizuri lakini hauwezi kuwepo, Rais
hakutoa vitisho bali mawazo yake kama Mtanzania, hawa jamaa wamekubaliana,
serikali ya Znz wachukue CUF, bara CHADEMA na muungano waachiwe CCM’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MH LUKUVI AJIBU MAPIGO YA WAPINZANI BUNGENI KUHUSU KAULI YA JESHI KUTAWALA NCHI.”
Post a Comment