Thursday, April 17, 2014

TAYARI VIJANA 16 WA TIMU YA MABORESHO WAPATIKANA TFF YAWAWEKA HADHARANI MBEYA.








JOPO la Makocha wa Timu ya Maboresho waliweka kambi Mjini Tukuyu Rungwe Mbeya  limetangaza majina ya wachezaji 16 waliopataikana katika mchakato wa maboresho ya timu mpya ya taifa ya Tanzania.

Vijana hao 16 ni kati ya 33 waliopatika katika mchakato wa kutafuta vijana wenye vipaji kwa lengo la kupata timu mpya ya Taifa mchakato ambao ulihusisha mikoa yote ya Bara na Visiwani ambapo kambi hiyo ilianza kuanzia Machi 22 mwaka huu .
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Hapa  Kocha Msaidizi wa Kikosi hicho ca Maboresho Ndugu Salum Mayanga amesema teyari hatua ya awali ya kuwapata vijana 16 imekwisha fanyika wakati wakiwa kambini hapo Mjini Tukuyu Mbeya.

Amewataja wachezaji waliochaguliwa katika mchakato huo kwa upande wa walinda mlango kuwa ni  Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara).

Kwa upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba),  Omari Kindamba (Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).
Mabeki wa kati ni Yussuf Suleiman Mlipili (Temeke)Abbas  na Said Juma Ali (Mjini Magharibi)huku Viungo wakiwa ni
 Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga).

Huku viungo wa pembeni ni Ommar Athuman Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara)
Washambuliaji ni  Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara ,(Ilala) Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba),
Hata hivyo amesema wachezaji wengine waliungana na wale 16 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga)na Bayage Atanas Fabian (Mbeya)kutoka timu ya vijana wenye umri (160)

Amesema Wachezaji hao 16 wataungana na wale wa Taifa Stars watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
                     
Pamoja na kutaja kikosi hicho pia amesema kuwa katika wale vijana walienguliwa katika kikosi hicho Tayari TFF imewaka utaratibu mzuri namna ya kuwatumia kwa hapo baadaye na pale watakapo hitajika.
                                                                                                                                                     
Timu hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na makocha Hafidh Badru, Salum Mayanga na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu utafanyika mchujo ili kupata wachezaji wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa Stars watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
MWISHO
 

0 Responses to “TAYARI VIJANA 16 WA TIMU YA MABORESHO WAPATIKANA TFF YAWAWEKA HADHARANI MBEYA.”

Post a Comment

More to Read