Monday, April 21, 2014

MBEYA CITY FC UTANI MWIKO, MAANDALIZI YA MSIMU UJAO YAIVA!!.





TAARIFA zilizotufikia asubuhi ni kwamba benchi la ufundi la Mbeya City fc chini ya kocha mkuu, Juma Mwambusi akisaidiwa na Maka Mwalwisyi linatarajia kufanya kikao mchana wa leo kwa lengo la kutathmini walichovuna msimu huu.

Kocha msaidizi wa Mbeya City, Maka Mwaliwisyi ameuambia mtandao huu kuwa wamefurahishwa na mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika msimu wao wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara, ingawa malengo yao ya kutwaa ubingwa hayajatimia.

“Mchana wa leo sisi kama benchi la ufundi tunakutana ili kutathmini kile tulichokipata”.
“ Kulikuwepo na changamoto nyingi na tumemaliza nafasi ya tatu”.

“Tunakaa kwasababu tunatakiwa kuwasilisha ripoti mapema ili kuendelea na maandalizi ya timu”. Alisema Maka.

Kuhusu usajili, Maka alisema hawatahangaika na wachezaji wenye majina kwasababu falsafa yao inawabana.

“Wachezaji wetu wanatutosha. Tutapata wengine kwa njia ile ile tuliyotumia”.
“ Falsafa yetu inasema lazima tuwatoe wachezaji chini na kuwapandisha juu. Tukisema tutamani basi tutapotea njia yeti tuliyoianzisha”
“Hawa tulionao tutabaki nao ili tuone falsafa yetu itatufikisha wapi. Hatusajili wachezaji wenye majina na ndivyo ilivyo kwa Mbeya City fc”. Aliongeza Maka.

Mbeya City imekuwa timu bora msimu huu kwa kuleta changamoto kubwa kwa klabu za Simba, Yanga na Azam fc.

Katika msimu wake wa kwanza, wamewachomoa Simba katika nafasi tatu za juu.
Wamemaliza ligi katika nafasi ya tatu kwa pointi 49, huku nafasi ya nne ikiangukia mikononi mwa Simba kwa pointi 38.
Mwa jana, Yanga walitwaa ubingwa, Azam fc nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu, Kagera Sugar nafasi ya nne.
Lakini mwaka huu Azam fc wametwaa ubingwa, nafasi ya pili Yanga, Mbeya City fc ya tatu, Simba ya nne, na Kagera Sugar imeporomoka mpaka nafasi ya tano.

Timu nyingine zilizopanda na Mbeya City fc, kwa maana ya Ashanti United na Rhino Rangers zimeshashuka daraja sambamba na JKT Oljoro.

Sasa nafasi zao zimechukuliwa na Stand United ya Shinyanga, Ndanda fc ya Mtwara na Polisi Morogoro ya Mkoani Morogoro.

0 Responses to “MBEYA CITY FC UTANI MWIKO, MAANDALIZI YA MSIMU UJAO YAIVA!!.”

Post a Comment

More to Read