Monday, April 21, 2014
MOYES MWENDO MDUNDO KUBOMOA REKODI ZA MAN UNITED!!.
Do you like this story?
MASHETANI wekundu, Manchester United
wamekuwa na msimu mbaya mwaka huu tangu David Moyes aingie Old Traffod kurithi
mikoba ya Sir Alex Ferguson na sasa anaendelea kuvunja rekodi mbalimbali
klabuni hapo.
Baada ya kufungwa mechi ya jana mabao
2-0 na Everton uwanja wa Goodison Park, Man United hawawezi kumaliza ligi
katika nafasi ya nne na kwa maana hiyo watakosa michuano ya UEFA kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 1995.
Ushindi wa jana uliwafanya Everton kwa
mara ya kwanza kushinda nje ndani dhidi ya Man United tangu mwaka 1969-70.
Hapo chini ni orodha ya rekodi
zilizovunjwa na Moyes ambazo zilichapishwa na mtandao wa Goal.com baada ya Man
United kulala mabao 3-0 dhidi ya Manchester City mwishoni mwa mwezi machi
mwaka huu, lakini Moyes amendelea kuvunja rekodi zingine msimu huu
|
|
United kwa mara kwanza wanamaliza
ligi wakiwa nafasi ya chini tangu ligi kuu England kuanzishwa.
|
|
|
United wanashindwa kufuzu michuano ya
UEFA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995
|
|
|
United wamefanya vibaya zaidi
nyumbani baada ya miongo kadhaa kupita
|
|
|
Wamefungwa mara tatu mfululizo msimu
huu tangu 2001.
|
|
|
Wametolewa raundi ya tatu katika
kombe ka FA Cup kitu kilichotokea mara moja wakati wa Ferguson
|
|
|
Kufungwa kwa mara ya kwanza na
Swansea City wakiwa Old Trafford.
|
|
|
Kufungwa kwa mara ya kwanza nyumbani
na Newcastle tangu mwaka 1972
|
|
|
Kufungwa kwa mara ya kwanza nyumbani
na West Brom tangu 1978
|
|
|
Mechi ya kwanza ya ligi kupoteza
dhidi ya Stoke tangu mwaka 1984
|
|
|
Mara ya kwanza kwa Man United
kufungwa bao la mapema zaidi ligi kuu –bao la Dzeko walipokabiliana na
Manchester City
|
|
|
Mara ya kwanza kwa Man City na
Liverpool kumpiga nje ndani Man United Tangu Premier League kuanza
|
|
|
|
|
|
Mara ya kwanza Everton kumfunga Man
United nje ndani tangu mwaka 969-70
|
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “MOYES MWENDO MDUNDO KUBOMOA REKODI ZA MAN UNITED!!.”
Post a Comment