Monday, April 21, 2014
NDUGU WA WALIOZAMA NA MELI HUKO KOREA KUSINI WAPAMBANA NA POLISI.
Do you like this story?
Jamaa wa baadhi ya waathiriwa 250 wa ajali ya Ferry nchini Korea Kusini ambao bado hawajapatikana, wamekabiliana na polisi.
Jamaa hao wanalalamikia kile wanachosema ni kujikokota kwa waokozi wanaowatafuta waathiriwa hao.
Usiku kucha, wapiga mbizi walipata miili 17 zaidi baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya Ferry hiyo iliyozama kwa mara ya kwanza.
Walinzi wa bahari katika pwani ya nchi hiyo, walishindwa kueleza ni sehemu gani hasa ambapo miili hiyo ilipatikana ndani ya ferry hiyo baada ya kushindwa kuona vyema wakiwa chini ya bahari.
Meli hiyo ilizama siku ya Jumatatu ikiwa imewabeba watu zaidi ya mia nne wengi wakiwa wanafunzi wa shule.
Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa inaathiiri shughuli ya kuwatafuta waathiriwa.
Waendesha mashitaka wanasema kuwa wakati wa ajali hiyo kulikuwa na nahodha mwingine asiye na uzoefu aliyekuwa ameshikilia usukani wa meli hiyo.
Nahodha huyo alikamatwa pamoja na nahodha wa ferry hiyo na wafanyikazi wengine.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)

.gif)

0 Responses to “ NDUGU WA WALIOZAMA NA MELI HUKO KOREA KUSINI WAPAMBANA NA POLISI.”
Post a Comment