Tuesday, April 8, 2014

MTO KIKAMBA UMEKUWA TISHIO KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA UDINDE CHUNYA.








Picha na Fahari News


Wakazi wa kijiji Cha Udinde Kata ya Kapalala Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwajengea Daraja katika Mto Kikamba ambao umekuwa ukihatarisha maisha yao kwa kuwa na mamba wengi.

Wakizungumza na Fahari News blog  baadhi ya wananchi hao wamebainisha kuwa mto huo umekuwa ukihatalisha maisha yao kwa muda mrefu hasa katika kipindi cha mvua ambapo maji hufurika  hivyo kusababisha mamba kuzagaa ovyo.

Wamesema, mamba hao wamekuwa wakileta madhara kwa binadamu kwani hivi karibuni mwanamke mmoja  Yulita Sipiliano(54) mkazi wa Kijiji cha manda chini karibu na Ziwa Rukwa amepoteza maisha baada ya kutafunwa na mamba.


Sisi tunaiomba serikali itujengee daraja katika mto huu kwani watu wamekuwa wakitumia mitumbwi kuvuka  ambayo ni hatari kwa maisha ya watu hususani wanafunzi,”amesema Alex Martin mkazi wa Kijiji cha Udinde.


Amesema, pia wakinamama wajawazito wamekuwa wakijifungulia njiani  kutokana na kuchelewa kupata huduma ya usafiri  ambayo kwa asilimia kubwa imekuwa ikitolewa na waendesha mitumbwi.

“Wanawake wajawazito wanapata tabu sana hasa nyakati za usiku kwani waendesha mitumbwi wengi wamekuwa wamelala hivyo baadhi yao hujikuta wakipoteza maisha  pamoja na watoto wao,”amesema.

Kufuatia hali hiyo ameiomba serikali kuhakikisha inafanya mpango wa haraka katika kumaliza changamoto hiyo kwani daraja hilo ndio mkombozi kwao.

0 Responses to “MTO KIKAMBA UMEKUWA TISHIO KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA UDINDE CHUNYA.”

Post a Comment

More to Read