Wednesday, April 16, 2014
SIMBA YAJIFICHA ZANZIBAR KUTAFUTA SUMU YA KUWAUA YANGA JUMAMOSI!!.
Do you like this story?
WEKUNDU wa
Msimbazi Simba sc wamesahau vipigo vyote vya mechi za nyuma na sasa wameelekea
visiwani Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga SC aprili 19
mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu
wa Simba sc, Ezekiel Kamwaga ameuambia mtandao huu dakika chache zilizopita
kuwa kikosi cha wachezaji 18 kimeondoka jioni hii kwenda Zanzibar kutafuta sumu
ya kuwaua Yanga.
“Timu ipo
katika hali nzuri. Yaliyopita si ndwele, sasa akili yetu ni mchezo wa jumamosi
dhidi ya mtani. Tuna matarajio makubwa ya kushinda mechi hiyo”. Amesema
Kamwaga.
Kamwaga
amewatoa hofu mashabiki wa Simba ambapo amewahakikishia kuwa maandalizi
wanayoenda kuyafanya ni ya hali ya juu.
“Tumefanya
vibaya msimu huu kinyume na matarajio ya mashabiki wetu”.
“ Kuwafunga
Yanga mechi ya mwisho itakuwa faraja kubwa kwao. Uongozi umejiandaa vizuri na
timu ipo katika hali nzuri kabisa”. Ameongeza Kamwaga.
Hata hivyo
taarifa zilizoenea mchana wa leo ni kuwa wachezaji wa Simba waligoma kwenda
Zanzibar wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya mwezi huu.
Mwenyekiti wa
kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe alilazimika kuwalipa fedha
wachezaji wote na benchi la ufundi ili kuokoa jahazi, na jioni hii safari
ilianza.
Simba sc
wataingia uwanjani wakiwa na malengo ya kushinda na kulinda heshima yao.
Kocha mkuu wa
klabu hiyo, Dravko Logarusic alikaririwa na mtandao huu akisema mechi ya mwisho
ameipa uzito wa hali ya juu, hivyo alihitaji kambi kuwepo maeneo tulivu.
Mechi hiyo
haitakuwa na presha kubwa kwani matokeo kwa timu zote hayatabadili chochote kwa
maana ya Simba kupanda nafasi za juu wala Yanga kuchukua ubingwa.
Yanga wapo
nafasi ya pili kwa pointi 55 baada ya kucheza mechi 25, pointi nne nyuma ya
Azam fc waliopo kileleni kwa pointi 59, huku tayari wakiwa wameshajitangazia
ubingwa kwasababu hakuna klabu inayoweza kuzifikia pointi hizo.
Wachezaji
waliondoka jioni hii ni walinda mlango Ivo Philip Mapunda na Yaw Berko.
Walinzi ni
William Lucian ‘Gallas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ Joseph Owino, Donald Mosoti,
Nassor Masoud ‘Chollo’.
Viungo Henry Joseph, Ramadhani Chombo ‘Redondo’,
Uhuru Suleiman Jonas Mkude, Said Ndemla, Awadh Juma, Ramadhani Singano ‘Mesi’,
Haroun Chanongo, Amri Kiemba na washambuliaji ni Amisi Tambwe na Zahor Pazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA YAJIFICHA ZANZIBAR KUTAFUTA SUMU YA KUWAUA YANGA JUMAMOSI!!.”
Post a Comment