Wednesday, April 16, 2014

TANESCO MBEYA YAMKAMATA MWIZI WA UMEME.



Mkuu wa usalama wa TANESCO Mkoa wa Mbeya.


Huyu ndiye Mtuhumiwa





Hii ndio Sehemu aliyokuwa akiiba Umeme katika mita ya Ruku




Shirika la Umeme Tanesco Mkoani Mbeya bado linakabiliwa na Tatizo la kuwepo kwa mafundi umeme feki wa mitaani ambao wamekuwa wakiunganishia wananchi huduma hiyo hali ambayo imelifanya shirika hilo kuingia hasara kubwa.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kuwepo kwa msako unafanywa na shirika hilo Mkoani Mbeya na maeneo mengine kwa ujumla  lengo la kubaini watu wanaolihujumu shirika hilo.

Afisa Usalama mwandamizi wa shirika hilo kwa Mkoa wa Mbeya Ndugu Siprian Lugazia amesema vitendo vya kuliibia shirika kwa kujiungnishia umeme majumbani vimeanza kuibuka upya katika kipindi cha kuanzia mwezi January hadi Aprily kwa baadhi ya maeneo mkoani humo.

Amesema wamekuwa wakipata taarifa mbalimbali toka kwa baadhi nya wananchi juu ya kuwepo  kwa vitendo hivyo.

Amesema mara baada ya kufuatilia taarifa hizo walibaini kuwepo kwa hali hiyo kwa baadhi ya wateja wao ambao hata hivyo baadhii yao walikili   kufanya udanganyifu huo huku baadhi yao wakidai kuunganishiwa na mafundi wa mitaani .

Hata hivyo amefafanua kuwa hivi karibuni wamekamata mmoja wa wajasilimali wawanaojihusisha na uchomeleaji katika eneo la Ilomba jijini mbeya na kumchukulia hatua za kisheria
Hata hivyo Afisa huyo amesema msako huo utaendelea kufanyika mara kwa mara kwa lengo la kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Mwisho.

0 Responses to “TANESCO MBEYA YAMKAMATA MWIZI WA UMEME.”

Post a Comment

More to Read