Thursday, May 15, 2014
MTOTO AANGUKA TOKA GOROFA YA 11 ANUSURIKA.
Do you like this story?
Mtoto
mwenye umri wa mwaka mmoja amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka orofa ya
11 ya jengo moja mjini Minnesota Marekani.
Vyombo
vya habari katika jimbo hilo vimeripoti kuwa Musa Dayib, amevunjika mkono mara
mbili na kwa sasa anapumua kwa usaidizi wa mashine japo madaktari wanamtarajia
kuishi.
Musa
aliteleza katikati ya mianya inayozingira sebule yao katika orofa ya 11 ya
mjengo huo wenye nyumba na makazi ya watu.
Muuguzi
mkuu katika zahanati aliyolazwa amesema kuwa Musa anatarajiwa kuishi baada ya
kuanguka katika eneo lisilo kavu sana.
Jamaa
na marafiki wa familia hiyo ya kisomali wamepigwa na butwaa kutokana na tukio
hilo.
Tukio
hilo lilizua mjadala kama ni muujiza au la kuwa amenusurika kifo lakini
watafiti wameelezea kuwa mtoto ananafasi nzuri zaidi ya kuishi hata baada ya
kuanguka ama kupatwa na janga lolote lile kwani mwili wao bado ni mwororo na
mifupa ya mtoto huwa bado ni laini kinyume na mtu mzima ambaye tayari mifupa
yake ni kavu na mwili wake ni mkubwa na mzito.
Abdirizak
Bihi alisimulia muujiza huo kwa gazeti la The Star-Tribune .
"baada
ya kushuhudia yaliyotendeka hapa ninahofia usalama wa wazazi wa mtoto ambao
hadi kufikia sasa wamepigwa na bumbuazi hawazungumzi na yeyote."
Dakta
Tina Slusher, aliyemhudumia mtoto Musa, alisema hakuna vile mtu mzima
angenusurika baada ya kuanguka umbali kama huo.
Bila
shaka huu ni muujiza wa Mwenyezi mungu kwa familia hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTOTO AANGUKA TOKA GOROFA YA 11 ANUSURIKA.”
Post a Comment