Wednesday, May 14, 2014

PLUIJM AWAPA RAHA YANGA.




KOCHA mkuu wa yanga hans van der pluijm anatarajia kuagwa kesho katika sherehe zitakazofanyika jijini dare s salaam tayari amenza utekelezaji wa ahadi yake na kuipatia timu hiyo wachezaji baada ya kupata wachezaji wawili nchin Ghana.

Pluijm aliyeingia yanga msimu uliopita na kuiwezesha kumaliza ligu kuu kwa nafasi ya pili tayari mkataba wake  wa miezi sita umekwisha  na amekwenda  katika timu inyoshiriki ligi kuu nchini  Saudi Arabia  ya al schoolah FC ambapo tayari aalisaini mkataba  wa mwaka mmoja.

Wiki iliyopita pluijm alisema kabla ya kwenda kuwatumikia waarabu  hao ataifanyia kazi taarifa ya benchi la ufundi kwa kufitafutia yanga wachezaji wakali watakaosaidia timu hiyo kufanya vizuri msimu ujao.

Baada ya kusaini mkataba wake  nchini Saudi Arabia kocha huyo raid wa uholanzi amerejea dare s saalam mwishonimwa wiki , na uongozi  umethibitisha  hilo na kueleza kuwa anatarajiwa kuangwa kesho katika sherehe fupi zitazofanyika  kwenye makao makuu ya yanga. Jangwani.

0 Responses to “PLUIJM AWAPA RAHA YANGA.”

Post a Comment

More to Read