Wednesday, May 14, 2014

MATOKEO CHANJO YA UKIMWI LEO.




MATOKEO ya utafiti wa chanjo ya ugonjwa wa ukimwi  na magonjwa yasiyoambukiza nchini  yatatolewa katika kongamano  la kisayansi linaloanza  leo jijini dare s salaam.

Kongamano hilo la siku mbili lenye kaulimbiu  ya utafiti  wa afya , mafunzo  na ubunifu kwa maendeleo  endelevu limeandliwa na chuo kikuu cha afya na sanyansi shirikishi muhimbili(muhas).

Kaimu mkuu wa chuo hicyo profesa eligius lyamuya lisema  juzi dare s salam kwamba utafiti huo utatolewa mbele ya wanasayansi washiriki 350 toka nchi tisa duniani  ambao watatumia jongamano hili kubadilishana  ujuzi na uzoefu katika ufanyaji utafiti.

Mada zaidi 138 zinatarajiwa  kuwasilishwa katika kongamano hilo ambapo kati ya hizo mada 122  zitawasilishwa  kwa njia yam domo ikiwamo ya utafiti wa chanjo ya ukimwi pamoja na magonjwa yasiyoambukiza.

Majaribio yaliyopita
Mwaka jana kiongozi wa jopo hilo la wataalamu  wa mhas wanaofanya utafuti huo profesa Muhammad bakari alitoa ufafanuzi kuhusu majaribio ya chanjo hiyo akisema bado walikuwa wakiendelea kuifanyia utafiti zaidi.

Profesa bakari alikaririwa akisema majaribio ya chanjo hiyo yalifanyika nchini  mwaka 2007 mpaka 2010  na 2008 mpaka 2012 yalionyesha mafanikio mazuri ingawa hayakufikia hatua ya kupatkana kwa chanjo kamili.

Kwa mujibu wa profesa bakari  majaribia hayo yalithibitisha kuwa chanjo YA DNA-MVA ilikuw salama na yenye uwezo  wa kuufanya mwili utengeneze kinga dhidi ya virusi vya ukimwi (VVU)

Pamoja na matokeo hayo ya kutia moyo baada ya kuanza kufanya utafiti jopo la madaktari bado liliendela na utafiti zaidi kuanza 2008 hadi 2012 ili kupata chanjo.

Hatukuishai hapo utafiti  wa pili (TAMOVAC-01) ulifanyika kati ya 2008 na 2012  utafit huu ulijumuisha  pia nchi jirani ya msumbiji alisema .

Alisema utafit wa awali ambao ulijulikana HIVIS-03 ulihusisha aksari 60 ambao walifuatiliwa kwa karibu  wakti wote wa utafiti  ili kuhakiki usalama wa chanjo na uwezo wa chanjo kutengeneza vichocheo vya kinga dhidi ya  VVU.

0 Responses to “MATOKEO CHANJO YA UKIMWI LEO.”

Post a Comment

More to Read