Wednesday, May 14, 2014
USIOMBEE KUUGUA DENGUE,KIPIMO SH 50,000.
Do you like this story?
Wakati
taharuki iliyosababishwa na mlipuko wa homa ya dengue ikiendelea kutikisa kila
kona ya jiji, imebainika kwamba gharama za vipimo katika hospitali mbalimbali
zinafikia Sh50,000, ikiwa ni tofauti kubwa na Sh1,000 kwa kipimo cha malaria.
Ugonjwa
huo unazidi kusambaa jijini Dar es salaam na baadhi ya mikoa, kiasi cha mamlaka
kuagiza mabasi yote yaendayo mikoani yafanyiwe usafi wa kunyunyizia dawa za
kuua wadudu kudhibiti usienee zaidi mikoani. Pia wananchi wameshauriwa kuvaa
nguo ndefu ili kudhibiti mbu wanaoeneza ugonjwa huo mchana tofauti na mbu wa
malaria.
Timu
ya waandishi wa Mwananchi ilipita katika baadhi ya hospitali kubwa binafsi na
za Serikali jijini Dar es Salaam na kubaini kuwa gharama ya kupima homa hiyo ni
kubwa zaidi katika hospitali na vituo binafsi vya afya, lakini wagonjwa
wanaokwenda katika hospitali za Serikali hulazimika kulipa kati ya Sh25,000 na
Sh30,000. Pamoja na homa hiyo kufananishwa na malaria kwa dalili na kuenezwa na
mbu, gharama za vipimo vyake ni tofauti kwani mgonjwa wa malaria hutozwa kati
ya Sh1,000 na 2,000.
Hata
hivyo, jambo la kutia moyo ni kwamba baada ya mgonjwa kupata majibu na
kubainika anaumwa homa ya dengue, gharama za tiba huwa ndogo kati ya Sh200 na
500 za kununulia dozi ya dawa za kutuliza maumivu aina ya panadol.
Wanaopima
waongezeka
Mchunguzi
wa magonjwa katika maabara ya kimataifa ya Lancet, Kanda ya Tanzania, Mohamed
Abdulai alisema idadi kubwa ya watu wanakwenda katika maabara hiyo kupima homa
ya dengue tangu ugojwa huo uenee kwa kasi kati ya Machi na Aprili mwaka huu.
Alisema
kwa siku wagonjwa zaidi ya 40 hupima dengue na katika kipindi kisichozidi mwezi
mmoja, wagonjwa 53 waligundulika kuwa na homa hiyo.
Abdulai
alisema gharama za kipimo cha dengue katika kituo hicho ni Sh50,000.
Katika
Hospitali ya Aga Khan, Mkurugenzi wa Tiba, Dk Jaffer Dharsee alisema kipimo cha
homa ya dengue ni kati ya Sh35,000 hadi Sh40,000 kutokana na mchakato wa
upimaji wake.
“Ni
lazima tunapompima mtu dengue pia tumpime na maradhi mengine kwanza kama homa
ya matumbo, malaria na maradhi mengine ambayo tunahisi anayo na ndiyo gharama
inakuwa kubwa,” alisema Dk Dharsee.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Hindu Mandal, Dk Kaushik Ramaiya alisema katika hospitali hiyo
kipimo cha homa ya dengue ni Sh30,000. “Tunatumia vipimo vitatu, kile
kitakachoangalia iwapo chembe hai nyeupe za damu zimepungua, malaria na kiwango
cha sumu kinachotokana na virusi vya dengue,” alisema.
Dk
Ramaiya alisema tangu vyombo vya habari vianze kuripoti ugonjwa huu, watu
wamejawa hofu na hufika hospitali kwa wingi wakitaka kupima maradhi hayo ili
kujua kama wapo salama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “USIOMBEE KUUGUA DENGUE,KIPIMO SH 50,000.”
Post a Comment