Wednesday, May 14, 2014
WABUNGE WAPITISHA MSWAADA,UKIMWAMBUKIZA MTU VIRUSI VYA UKIMWI KWA MAKSUDI UNAFUNGWA JELA MIAKA 10
Do you like this story?
Wabunge nchini Uganda wamepitisha
mswaada unaotoa adhabu kali kwa watu wanaowaambukiza wengine virusi vya HIV kwa
maksudi.
Mswada huo unapendekeza adhabu ya
kifungo cha hadi miaka 10 kwa wale wanaopatikana na hatia na pia inapendekeza
wanawake wajawazito na wapenzi wao kupimwa virusi vya HIV.
·
Mbunge mmoja kwa jina Peter Aleper
aliambia vyombo vya habari kuwa watu wanaowaambukiza wenzao virusi vya HIV kwa
maksudi ni hatari kwa jamii.
"ni lazima waadhibiwe vikali kwa
sababu kumuambukiza mtu HIV wakati unafahamu vyema kuwa wewe ni mwathiriwa ni
uhalifu,'' alisema mbunge huyo. Ni hatari sana kwa sababu mtu huyo anaweza
kuichanganya jamii na kumaliza watu.''
Lakini wafanyakazi katika sekta ya afya
pamoja na mashirika ya kutetea haki za wanyonge, wamepinga vikali mswada huo,
wakisema kwamba haitafanya lolote kudhibiti ongezeko la visa vya maambukizi.
Wengi wanasema kuwa mswada huo
utaongeza tu unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi hivyo. Pia wanasema kuwa
watu watahofia kupimwa kwa hofu ya kutengwa na jamii.
Mswada wenyewe umepitishwa baada ya
sheria kali inayopinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupitishwa na rais
Yoweri Museveni mwezi Februari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ WABUNGE WAPITISHA MSWAADA,UKIMWAMBUKIZA MTU VIRUSI VYA UKIMWI KWA MAKSUDI UNAFUNGWA JELA MIAKA 10 ”
Post a Comment