Thursday, June 19, 2014
KIASI KINGINE CHA GESI CHAGUNDULIKA NCHINI.
Do you like this story?
Kampuni
ya Statoil ya Norway na mshirika wake ExxonMobil wamegundua kiasi kingine
kikubwa cha gesi katika Bahari ya Hindi nchini Tanzania.
Kiwango
hicho kinakadiriwa kufikia futi za ujazo trilioni mbili mpaka tatu (sawa na
lita trilioni 56.6 hadi trilioni 84.9).
Ugunduzi
huu unafanya jumla ya ujazo wa gesi iliyogunduliwa na washirika hao kufikia
takriban futi za ujazo trilioni 20 (lita trilioni 566.25) kwenye Kitalu Namba
2, ambako washirika hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji.
‘’Tangu
mwaka 2012 tumekuwa tukipata mafanikio ya asilimia 100 nchini Tanzania na eneo
hilo limekuwa kitovu cha utafiti ndani ya muda mfupi. Ni kwa haraka tulitoka
kwenye kuchimba kisima kimoja hadi kuwa na mkakati wa kuchimba visima vingi,’’
alisema Makamu wa Rais wa Shughuli za Utafiti za Statoil Ukanda wa Magharibi,
Nick Maden.
Ugunduzi
huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango kidogo cha
mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi katika Kisima cha
Zafarani-1 mwaka 2012.
Ugunduzi
katika kisima hicho unakuwa wa sita katika Kitalu Namba 2.
Uchimbaji
wa gesi katika kisima hicho ulifanywa na meli ya Discoverer Americas, usawa wa
mita 2,360 za kina cha maji. Meli hiyo sasa inachimba kisima kingine cha
Binzari katika Kitalu namba 2
Statoil
ambayo imekuwapo nchini tangu 2007, inatafiti na kuchimba gesi katika kitalu namba
mbili kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na
hisa ya asilimia 65 katika kitalu hicho wakati ExxonMobil Exploration and
Production Tanzania Limited ina asilimia 35.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIASI KINGINE CHA GESI CHAGUNDULIKA NCHINI.”
Post a Comment