Thursday, June 19, 2014

KIKWETE AKABIDHI BODABODA 10 KWA UWAPA ARUSHA



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta,Jakaya Kikwete,jana alikabidhi msaada wa Pikipiki10 kwa chama cha  Akiba na Mikopo   cha  Waendesha Pikipikikatika jiji la Arusha,UWAPA SACCOS, zenye thamani ya shilingi  milioni
15.9
Pikipiki hizo zimekabidhiwa
 kwa uongozi  wa  Umoja  wa  Waendesha Pikipiki Jiji
la Arusha (UWAPA) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo katika hafla
iliyofanyika katika viwanja  vya Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa
Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi
yake ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa  waendesha boda boda hao
wakati akihutubia mkutano wa hadhara Novemba mosi mwaka 2012 kwenye uwanja wa
Sheikh Amri Abeid  wakati wa ziara ya Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Magesa
Mulongo  amesema ajali za pikipiki mkoani humo zimepungua kutokana na
waendesha pikipiki hizo kupewa mafunzo na hivyo kuzingatia sharia za usalama
bara barani tofauti na hapo awali.
Amewapongeza waendesha
 bodaboda hao ,  kwa kuanzisha vituo vyao ambavyo kwa sasa
vinafahamika na tayari vimeshasajiliwa na kuwataka waviimarishe katika swala
zima la ulinzi na usalama wa abiria.
Mulongo, amesema kuwa waendesha boda
boda hao wamekuwa wakichangia sana kuimarisha maswala ya usalama na hivyo
matukio makubwa ya uhalifu yamepungua sanjari na matukio ya kujichukulia sharia
mkononi.
Amesema msaada huo ni mtaji  wa
kuendeleza Saccos hiyo ,na akaahidi kuwanunulia Jacket 1000 ambazo ni sale ili
watambulike .
Mulongo,akawataka wasijihusishe na
vurugu ,wasikubali kugeuzwa kuwa ni sehemu ya  kufanya vituko na vitendo
vya uhalifu na uvunjifu wa amani.
Pia aliwataka wasikubali kutumiwa na
kugeuzwa  nabaadhi ya watu ili wasitumbukie na  kushabikia mambo
yasiyofaa kwa jamii ikiwemo uhalifu .
Akisoma lisara, Katibu wa Uwapa
Saccos, Salvatory Massawe, amesema Sacoss hiyo ina wanachama 2300 na bado
milango iko wazi kwa waendesha boda boda wengine jijini Arusha kujiunga,kwa
kuwa Saccos hiyo ni kiungo muhimu .
Amesema kuwa tayari vituo 144
vimesajiliwa  na bado mchakato wa kusajili vituo vingine unaendelea lengo
ni ili viutambulike na kufahamika hivyo inakuwa ni rahisi kuzuia matukio ya
kihalifu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Saccos
hiyo, Godlight Rugemarila, alisema kuwa,boda boda zimetoa ajira nyingi na hivyo
kupunguza kwa kiwango kikubwa matukio ya uhalifu.
Hafla hiyo  pia imehudhuriwa na
Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na
Wilaya ya Arusha,watumishi katika Sekretarieti ya Mko  huo na Watendaji wa
Jiji la Arusha

0 Responses to “KIKWETE AKABIDHI BODABODA 10 KWA UWAPA ARUSHA”

Post a Comment

More to Read