Thursday, June 19, 2014
BASI LA NEW FORCE LAUA WIWILI MBEYA.
Do you like this story?
![]() |
![]() |
|
Mkuu wa mkoa wa mbeya Abasi Kandoro akipewa maelezo na polisi wa usalama barabarani
|
Watu wawili Watembea kwa miguu wawili waliotambulika kwa
majina ya Theresia Hiingi (65) Mary Kizito (26) wote wakazi wa igurusi wamefariki dunia baada ya kugongwa na
basi la kampuni ya usafirishaji – new force lenye namba za usajili t. 952 cgu aina ya scania lililokuwa
likiendeshwa na yahaya abdalah (39)
mkazi wa dsm.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 18.06.2014 majira ya saa
18:00 jioni katika kijiji cha igurusi, kata ya igurusi, barabara kuu ya mbeya/njombe, wilaya ya
mbarali, mkoa wa mbeya..
Inadaiwa kuwa basi hilo lililokuwa likitokea Dar es salaam
kuelekea mbeya mjini liligonga gari t. 954 amh aina ya fuso lililokuwa likiendeshwa na dereva tupa anyosisye (32) mkazi wa kiwira –tukuyu, kisha kuacha njia na kuwagonga
watembea.
Aidha katika ajali hiyo watu wengine wanne walijeruhiwa kati
yao abiria mwanaume mmoja na wanawake watatu watembea kwa miguu wote wamelazwa
katika hospitali ya misheni chimala.
Pia miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini hapo. Chanzo
cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa basi, ambaye amekimbia mara baada ya
ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Kufuatia hali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina
msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini
wanapotumia vyombo vya moto hasa kwa kuzingatia alama na sheria za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.
Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo
mtuhumiwa wa tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)












0 Responses to “BASI LA NEW FORCE LAUA WIWILI MBEYA.”
Post a Comment