Thursday, June 19, 2014

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAKAMATA SILAHA YA KIVITA.


Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi akionyesha silaha aina ya Ak 47 kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwake





Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya  limeua jambazi Joseph Kapinga Mkazi wa Mafiga Mkoani Morogoro akiwa  na silaha aina ya Ak 47 yenye risasi 25 kwenye magazine.

Tukio hilo limetokea June 19 mwaka huu majira ya saa 11 alfajili  ambapo askari polisi walikutana na watu waliowatilia shaka kutokana na jinsi walivaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jiji hapa Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa  taarifa za kuwepo kwa majambazi hao waliarifiwa na  walinzi  wa soko kuu la Tunduma .

Amesema  mara baada ya kupata taarifa hizo  askari waliokuwa doria walianza msako  mkali wa kuwatafuta watu hao.
Amesema  kutokana msako huo walifanikiwa kuwaona watu hao  wawili wakiwa wamevalia makoti makubwa  meusi  huku mwingine akiwa amebeba mfuko  mkubwa ambao unaadiwa ulikuwa silaha.

Kamanda Msangi amesema mara baada ya kuwaona   watu hao walisimamisha  ambapo walianza kukimbia na mmoja kati yao  aliyekuwa amevaa jaketi jeusi   alikimbia kwa umbali  wa  mita ishirini na kuanza kufyatua risasi hovyo huku akielekea eneo waliopo askari.

Amesema mara baada ya kuona  hali hiyo askari  walijibu mapigo na katika majibizano hayo  ya kulushiana risasi  jambazi Kapinga ambaye alikuwa akitumi bunduki aina AK.47  yenye  namba 592058 na yenye risasi 25 kwenye alikufa papo hapo.

Hata hivyo Msangi amebainisha kuwa katika tukio hilo  hakuna madhara  kwa wananchi  wara askari yaliyotokea  huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika  ikiwa ni pamoja na kuendelea kumtafuta jambazi mwingine.

0 Responses to “JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAKAMATA SILAHA YA KIVITA.”

Post a Comment

More to Read