Thursday, June 19, 2014
UCHAGUZI SIMBA KIMEELEWEKA, MALINZI AMWAGA `MISIFA` KWA ADEN RAGE
Do you like this story?
UCHAGUZI wa Simba sc kwa asilimia kubwa
utaweza kufanyika juni 29 kama ilivyopangwa kufuatia kauli ya Rais wa
shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi akimpongeza rais wa Simba
Ismail Aden Rage kwa kufanya juhudi ya kufanya mazungumzo na shirikisho hilo.
Akuzungumza mchana huu na waandishi wa
habari katika ofisi za shirikisho hilo zilizopo katikati ya jiji, Posta, Rais
Malinzi amesema tangu alipotangaza kusimamisha uchaguzi huo jumapili iliyopita
na kuwataka Simba kuunda kamati ya maadili itakayosikiliza masuala yao ya
maadili, rais wa Simba, Aden Rage amekuwa akiwasiliana naye vizuri na kwa
heshima ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Malinzi alisema wamekuwa na maelewano
mazuri na Rage, hivyo ana imani ufumbuzi utapatikana .
Maneno ya Malinzi yanatoa imani kuwa
yeye na Rage wameshafikia hatua nzuri na bila shaka uchaguzi utafanyika kama
ulivyopangwa.
“Nimpongeze sana mwenyekiti wa klabu ya
Simba pamoja na kamati yake ya utendaji, kuanzia siku ya jumapili hadi leo hii
tumekuwa tukiwasiliana kwa karibu sana, katika hali ya maelewano, heshima
kubwa”. Alisema Malinzi mchana huu.
“Na niseme tu kwamba leo mgombea mmoja
ambaye kamati ya uchaguzi ilimuondoa katika uchaguzi, sina haja ya kutaja
majina hapa, alileta rufaa yake, leo saa
nane mchana kamati ya rufaa inakaa”. Aliongeza Malinzi.
Malinzi alisisitiza kuwa baada ya zoezi
la leo la kusikiliza rufaa kukamilika, mazungumzo yataendelea baina ya TFF na
Simba kwa ajili ya ustawi wa soka la nchi hii.
“Baada ya hapo, vyovyote vile itakavyokuwa baada ya zoezi ya
leo, mazungumzo yataendelea baina ya TFF na klabu ya Simba, ni imani yetu
kwamba kwa ajili ya ustawi wa mpira wa nchi hii, kwa maana yoyote ile,
tunaamini ufumbuzi utapatikana”.
“Sasa ni ufumbuzi gani utapatikana,
siwezi kuuzungumzia sasa hivi, mimi nimeruhusu kwa maana ya shirikisho kwamba
kikao kifanyike leo cha kamati ya rufaa ya uchaguzi”.
“Na baada ya hapo, mazungumzo yataendelea
kuweza kuona ni kwa namna gani tutaweza kuwa katika hali nzuri ambayo itaweza
kuwasaidia ndugu zetu wa Simba wakaendeleza ustawi wa klabu yao”. Alisema
Malinzi”.
Mgombea aliyeenguliwa kwa mara ya pili
na kamati ya uchaguzi wa Simba chini ya mwenyekiti wake, Wakili Damas Daniel
Ndumbaro, Bwana Michael Richard Wambura amekata rufaa kupinga maamuzi hayo kwa
mara nyingine.
Kamati ya Ndumbaro ilimuondoa tena
Wambura kwa madai kuwa baada ya kurudishwa katika uchaguzi na kamati ya rufani
ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya aliongea
maneno ambayo ni kampeni kwenye vyombo vya habari wakati zoezi la kampeni bado halijaanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UCHAGUZI SIMBA KIMEELEWEKA, MALINZI AMWAGA `MISIFA` KWA ADEN RAGE”
Post a Comment