Saturday, June 7, 2014
MADEREVA WA UMMA WAGOMA BRAZIL.
Do you like this story?
Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili
kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta
ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao
Paulo.
Takriban
nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu
katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe
la dunia kuanzia alhamisi ijayo.
Wafanyakazi
hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.
Awamu
nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo
utaendelea kwa mda usiojulikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MADEREVA WA UMMA WAGOMA BRAZIL.”
Post a Comment