Friday, June 6, 2014
MAKAHABA KUTIMULIWA KUTOKA MJINI NAIROBI.
Do you like this story?
Bunge
la jimbo la jiji la Nairobi nchini Kenya limepiga kura kuwaondoa makahaba
katikati mwa mji mkuu.
Waakilishi
katika bunge hilo walilazimika kupiga kura mara tatu ili kufikia matokeo hayo.
Kwa mara mbili matokeo ya kura yalikuwa sare, lakini baada ya awamu ya tatu
kura ya ndio ikashinda.
Hoja
hiyo iliwasilishwa na mwakilishi Bi Jane Mwasia, ikitaka wakuu wa jimbo
kuwaondoa makahaba mara moja kutoka katikati kwa jiji la Nairobi.
Waakilishi
wanaume walipinga hoja hiyo mara tu ilipowasilishwa lakini mjadala ulipotokota,
wengi waliamua kupiga kura ya ndio wakati wengine wakijizuia.
Mjadala
huo nusura uzue makonde bungeni na kusababisha hisia mseto miongoni mwa
waakilishi hao.
Baadhi
ya waakilishi hao walipendekeza kuwa sehemu maalum itengewe makahaba hao baada
ya wao kundolewa katika barabara zilizo katikati mwa jiji.
"sina
tatizo na makahaba kwa sababu wengi wao hawana ajira. Kwa hivyo ni jukumu letu
kuwajengea sehemu ambako wataweza kuendeshea shughuli zao,'' alisema mmoja wa
waakilishi hao.
Mwakilishi
mwingine, Manoah Mboko alisema kuwa suluhu kwa makahaba sio kuwaondoa mjini
bali ni kuwaoa kwani sheria ya kuoa zaidi ya mke mmoja ilipitishwa maajuzi.
Aliongeza kwamba makahaba wanachangia pakubwa sana katika uchumi wa mji wa
Nairobi.
Mwakilishi
mwingine alizua kicheko aliposema kuwa dunia nzima ni kama soko na hivyo kila
mtu aruhusiwe kuuuza bidhaa zake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAKAHABA KUTIMULIWA KUTOKA MJINI NAIROBI.”
Post a Comment