Sunday, June 8, 2014
MBEYA CITY FC ZITENDEENI HAKI MILIONI 360 ZA BINSLUM, FANYENI HAYA KUKIMBIA `USWAHILI` WA SIMBA, YANGA
Do you like this story?
MBEYA CITY FC kwa mara ya kwanza
imepata udhamini wa mamilioni ya fedha baada ya Kampuni ya Binslum Tyre Company
Limited kumwaga kitita kirefa cha milioni 360 kwa miaka miwili.
Kampuni hii ina nia ya kuifanya klabu
hii kuwa bora zaidi katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara . Siku zote
ukifanya kazi kwa moyo wote, ukawekeza nguvu kubwa kutafuta mafanikio, mwisho
wa siku juhudi zako zinakulipa.
Msimu uliopita, Mbeya City walionesha
nguvu kubwa na mipango mizuri ya ndani na nje ya uwanja. Walicheza kwa
kujituma, kwa malengo na nidhamu kubwa. Timu hii ilikuwa bora kuliko timu zote
tatu zilizopanda ligi kuu kwa msimu uliopita.
Ashanti United na Rhino Rangers
ziliishia kuonja tu utamu wa ligi kuu na kurudi tena ligi daraja la kwanza.
Lakini kwa Mbeya City fc ilikuwa ni tofauti, walishindana mpaka dakika ya
mwisho na kumaliza katika nafasi ya tatu.
Waliwachomoa wakongwe, Simba sc katika
ushindani wa nafasi tatu za juu. Nidhamu ya wachezaji na kuwa na uchu wa
mafanikio, maandalizi ya muda mrefu, falsafa ya kocha Juma Mwambusi, hamasa ya
mashabiki, uongozi wenye mipango, ni miongoni mwa sababu chache kati ya nyingi
zilizowafanya Mbeya City wafike pale walipo.
Lakini kilio chao kilikuwa ni kukosa
udhamini. Viongozi walisikika mara nyingi wakisema wanaomba makampuni
mbalimbali kujitokeza kudhamini klabu. Haikuwa rahisi kupata udhamini kwasababu
ndio kwanza watu walikuwa wanapima upepo wake.
Hakuna mtu anayeweza kuwekeza pesa
sehemu ya hasara. Timu bora inang`ang`aniwa na wadhamini. Wala hakuna haja ya
kwenda kuwalilia wadhamini, wewe fanya mipango ya uwanjani, jenga timu ya
ushindani, ‘mipesa` itakuja yenyewe. Mafanikio ya Mbeya City yamemtekenya
Binslum na kumwaga milioni 360.
Ni pesa nyingi na endapo viongozi wa
klabu watakuwa makini kuzitumia, basi zitawasogeza mbele zaidi.
`Mipesa` ndio hiyo sasa, lakini
viongozi wa Mbeya City kumbukeni mambo machache yafuatayo;
Mosi; wachezaji wenu ndio chanzo cha
udhamini huo. Kumbukeni sio mkurugenzi wa jiji, wala katibu, wala mwenyekiti
aliyemvuta Binslum. Ni juhudi za Juma Mwambusi na benchi lake, pamoja na wachezaji wenu.
Ukali wa Paul Nonga, Mwegane Yeya,
Peter Mapunda, Steven Mazanda, Antony Matogolo, Deus Kaseke na wengineo ndio
chanzo cha kupata udhamini huo. Kwa maana hiyo, hawa vijana ndio walioleta
neema hiyo.
Cha msingi, wapeni haki zao. Kama
walikuwa wanalipwa kiasi kidogo, basi jaribuni kufikiria namna ya kuongeza dau.
Wamefanya kazi kubwa na wameona milioni 360, hivyo onesheni kuwajali na kuwapa
dau zuri. Haitakuwa jambo jema kubakia katika kiwango walichokuwa wanalipwa
awali, lazima mfanye `makeke` ili vijana waneemeke na jasho lao.
Sisemi ndio mtumie pesa zote kwao,lakini
angalau muoneshe kuwajali. Inakuwa mbaya sana unapozalisha pesa, wengine
wanafaidi. Inakatisha tamaa. Jitahidini kuboresha maslahi ya wachezaji.
Pili: siasa ndio adui mkubwa wa mpira
wa Tanzania. Wenzenu Simba na Yanga walianza kula matunda ya udhamini kwa miaka
mingi. Lakini sina hakika kama fedha hizo zimezinufaisha klabu. Nadhani tatizo
ni aina ya uongozi unaoziongoza klabu hizo. Kuna `waswahili` wengi na wachumia
matumbo. Watu wanaoingia katika klabu hizi wanajineemesha wao.
Kama kuna mtu ana uhakika, aseme ni
kiongozi gani amefanya kitu kikubwa na cha kihistoria kwa klabu hizi mbili.
Jibu ni hapana!. Bado uongozi ni tatizo kubwa. Hakuna watu wa kusimamia mapato
ya klabu, hawajapatikana watu wakutumia ipasavyo fedha za udhamini.
Watu wanajali maslahi binafsi, Ni timu
ambazo zinaendelea kutegemea fedha za watu wachache `mungu watu`.
Ili kufikia malengo yenu, epukeni na
siasa. Fanyeni kazi kwa malengo na kuzuia mianya ya kuibiwa kwa fedha zenu.
Tatu; boresheni kikosi chenu ili
kijitegemea. Moja ya malengo ya kocha Mwambusi ni kuwa na timu iliyojikamilisha
kwa kuzalisha wachezaji wake.
Soka la vijana ndio kila kitu.
Boresheni upande huo ili muwe na timu isiyochoka. Akichoka huyu mnapandisha
bunduki nyingine. Muwekeze huko bila kujali mafanikio yatapatikana lini.
Uvumilivu unahitajika, lakini itawalipa baadaye. Tumieni muda mwingi kubuni
namna ya kuboresha kikosi chenu kwa kujifunza kwa wenzenu walioendelea nje ya
nje.
Pia sajilini wachezaji kwa mipango ili
muwe na timu ya ushindani. Udhamini utakuja zaidi. Mwingine atakuja kuweka lebo
kwenye soksi tu, mwingine viatu, watang`ang`ania wenyewe. Lakini mkibweteka
basi mtamfukuza hata Binslum.
Mosi; wachezaji wenu ndio chanzo cha
udhamini huo. Kumbukeni sio mkurugenzi wa jiji, wala katibu, wala mwenyekiti
aliyemvuta Binslum. Ni juhudi za Juma Mwambusi na benchi lake, pamoja na wachezaji wenu.
Ukali wa Paul Nonga, Mwegane Yeya,
Peter Mapunda, Steven Mazanda, Antony Matogolo, Deus Kaseke na wengineo ndio
chanzo cha kupata udhamini huo. Kwa maana hiyo, hawa vijana ndio walioleta neema
hiyo.
Cha msingi, wapeni haki zao. Kama
walikuwa wanalipwa kiasi kidogo, basi jaribuni kufikiria namna ya kuongeza dau.
Wamefanya kazi kubwa na wameona milioni 360, hivyo onesheni kuwajali na kuwapa
dau zuri.
Haitakuwa jambo jema kubakia katika kiwango
walichokuwa wanalipwa awali, lazima mfanye `makeke` ili vijana waneemeke na
jasho lao. Sisemi ndio mtumie pesa zote kwao,lakini angalau muoneshe kuwajali.
Inakuwa mbaya sana unapozalisha pesa, wengine wanafaidi. Inakatisha tamaa.
Jitahidini kuboresha maslahi ya wachezaji.
Pili: siasa ndio adui mkubwa wa mpira
wa Tanzania. Wenzenu Simba na Yanga walianza kula matunda ya udhamini kwa miaka
mingi. Lakini sina hakika kama fedha hizo zimezinufaisha klabu. Nadhani tatizo
ni aina ya uongozi unaoziongoza klabu hizo. Kuna `waswahili` wengi na wachumia
matumbo. Watu wanaoingia katika klabu hizi wanajineemesha wao.
Kama kuna mtu ana uhakika, aseme ni
kiongozi gani amefanya kitu kikubwa na cha kihistoria kwa klabu hizi mbili.
Jibu ni hapana!. Bado uongozi ni tatizo kubwa. Hakuna watu wa kusimamia mapato
ya klabu, hawajapatikana watu wakutumia ipasavyo fedha za udhamini.
Watu wanajali maslahi binafsi, Ni timu
ambazo zinaendelea kutegemea fedha za watu wachache `mungu watu`.
Ili kufikia malengo yenu, epukeni na
siasa. Fanyeni kazi kwa malengo na kuzuia mianya ya kuibiwa kwa fedha zenu.
Tatu; boresheni kikosi chenu ili
kijitegemea. Moja ya malengo ya kocha Mwambusi ni kuwa na timu iliyojikamilisha
kwa kuzalisha wachezaji wake. Soka la vijana ndio kila kitu. Boresheni upande
huo ili muwe na timu isiyochoka. Akichoka huyu mnapandisha bunduki nyingine.
Muwekeze huko bila kujali mafanikio yatapatikana lini. Uvumilivu unahitajika,
lakini itawalipa baadaye. Tumieni muda mwingi kubuni namna ya kuboresha kikosi
chenu kwa kujifunza kwa wenzenu walioendelea nje ya nje.
Pia sajilini wachezaji kwa mipango ili
muwe na timu ya ushindani. Udhamini utakuja zaidi. Mwingine atakuja kuweka lebo
kwenye soksi tu, mwingine viatu, watang`ang`ania wenyewe. Lakini mkibweteka
basi mtamfukuza hata Binslum.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CITY FC ZITENDEENI HAKI MILIONI 360 ZA BINSLUM, FANYENI HAYA KUKIMBIA `USWAHILI` WA SIMBA, YANGA”
Post a Comment