Sunday, June 8, 2014
SIMBA WAVAMIA KIJIJI NA KUTAFUNA NG'OMBE ZAIDI YA KUMI HUKO KATAVI
Do you like this story?
Jumla ya
Ng’ombe kumi na Moja na mbuzi wanne
wameuwa na kuliwa na mnyama
simba katika matukio matatu tofauti yaliyotokea katika Tarafa
ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi baada
ya simba kuvamia katika vijiji vitatu
Kwa
mujibu wa Diwani wa Kata ya Mtapenda Elieza Fyula tukio la
kwanza lilitokea hapo Mei 28 majira
ya usiku katika Kijiji cha Kabatini
Katika
tukio hilo Simba walivamia kwenye
kijiji hicho na kuua na
kula Ng’ombe watatu na mbuzi watano ambao
walikuwa wako ndani ya zizi la kufugia mifugo .
Alisema siku iliyofuata
ya tarehe 29 meimajira ya usiku simba
hao walivamia katika Kitongoji cha
Kambike kilichoko katika Kijiji cha
Isinde na kuwauwa
Ng’ombe watano mali ya mfugaji wa kitongoji
hicho aitwaye Dirisha na kisha waliwala
ng’ombe hao.
DiwaniFyula alieleza baada ya
tukio hilo viongozi wa kitongoji walitoa taarifa kwa viongozi
wa kata ambao waliwasiliana na Idara ya Wanyama Poli ambao
waliwasili kijijini hapo na kuwaswaga simba hao wapatao watano.
Amesema
siku iliyofuata simba hao walivamia tena kwenye kijiiji cha
mkumbi na kisha waliuwa Ng’ombe wawili na kuwala
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA WAVAMIA KIJIJI NA KUTAFUNA NG'OMBE ZAIDI YA KUMI HUKO KATAVI”
Post a Comment