Wednesday, June 11, 2014

TAIFA STARS MZIGONI LEO KUWAWINDA `BLACK MAMBAS` KUSAKA TIKETI YA MOROCCO




IKIWA ni harakati ya kuikabili Msumbiji `Black Mambas` katika mchezo wa mwisho kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco, Taifa stars inatarajia kuingia tena kambini leo (Juni 11) mwaka huu.

Julai 20 mwaka huu, Taifa Stars itaanza nyumbani uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na wiki mbili baadaye itasafiri kwenda mjini Maputo kucheza mechi ya marudiano. Mshindi wa jumla ataingia hatua ya mwisho ya makundi.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.

Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.

0 Responses to “TAIFA STARS MZIGONI LEO KUWAWINDA `BLACK MAMBAS` KUSAKA TIKETI YA MOROCCO”

Post a Comment

More to Read