Friday, June 20, 2014

TRENI YA MWAKYEMBE YASITISWA KWA MUDA WA SIKU 3



. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imesitisha usafiri wa treni jijini Dar es Salaam kwa siku tatu kutokana na sababu za kiufundi.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, kaimu mkurugenzi mtendaji wa TRL, Mhandisi Elias Mshana alisema safari hizo zilisitishwa tangu jana. Amesema uamuzi huo ulifikiwa ili kufanya ukarabati wa injini za vichwa vya treni .

“Ukarabati unafanyika katika karakana kuu ya TRL iliyopo Morogoro, tunatarajia vichwa hivyo vitarejeshwa Dar es Salaam Jumapili,” amesema Mshana.

Amesema treni itaendelea na ratiba yake kuanzia Jumatatu ijayo

0 Responses to “TRENI YA MWAKYEMBE YASITISWA KWA MUDA WA SIKU 3”

Post a Comment

More to Read